Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 14, 2016

Zaidi ya Wakazi 4000 Kunufaika na Mradi wa Maji Wilaya ya PANGANI

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella katikati akipata maelezo ya mradi wa maji Boza-Kimang’a kutoka kwa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif wakati alipofanya ziara wilayani humo kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani,Esteria Kilasi.


 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti katikati akitazama mradi wa Maji  wa Boza-Kimang’a wa kwanza kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Ahmed.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti akiingia kwenye tanki la kuhifadhia maji.



ZAIDI ya wakazi 4009 wa Kijiji cha Boza Kimang’a wilayani Pangani Mkoani Tanga watanufaika na mradi wa huduma ya maji kupitia program ya maji na usafi wa mazingira vijijini (NRWSSP) katika mpango wa vijiji vya nyongeza.
Hayo yalisemwa juzi na Mhandisi wa Maji wilaya ya Pangani, Mohamed Seif wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji Boza-Kimang’a kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliyefanya ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.
Alisema kuwahadi sasa kisima kirefu kimekwisha kuchimbwa na usanifu wa mradi huo umefanyika na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji Saxon Building Contractor na kusimamiwa na Mtaalamu mshauri Don Consult Limited.
Mhandisi huyo alisema mradi huo ambao umeanza February 19 mwaka huu na kutarajiwa kukamilika Novemba 19 ukigharimu kiasi cha sh.milioni 884.4 ambapo shughuli zitakazofanyika ni uchimbaji wa kisima kirefu,ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia mashine,ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji.
Aliongeza kazi nyengine ni ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea
maji,kununua na kufunga mashine za kusukuma maji,kununua na kufunga mabomba ya viungio ikiwemo kuvuta umeme kwenye eneo hilo la mradi.
Akizungumza wakati akizundua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliwataka wananchi kuhakikisha  wanautunza vema ili uweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo ikiwemo kuacha kuharibu vyanzo vya maji.

0 comments:

Post a Comment