Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano huo.
“Tunachokifanya
ni kutoa huduma zaidi kuliko kufanya biashara kama Taasisi ya Serikali tukiwa
na dhamira ya kusaidia wananchi kuwa na visima na mabwawa yenye ubora
unaotakiwa”.Alisisitiza Egwaga
Akizungumzia
miradi iliyotekelezwa na Wakala huo, Egwaga amesema kuwa mpaka sasa Wakala
umekwishajenga mabwawa 23 katika kipindi cha januari 1997 hadi june,2016 katika
mikoa mbamimbali ikiwemo Tanga,Shinyanga, Tabora, Mtwara naPwani.
Akitaja
mikoa mingine ambako mabwawa hayo yamejengwa Egwaga alisema kuwa ni
Ruvuma,Manyara,Mbeya, mwanza, Lindi na Mara.
Akitoa mfano
wa miradi ya uchimbaji visima Egwaga alisema kuwa moja ya miradi iliyotekelezwa
ni ule wa kuchimba visima katika chuo Kikuu cha Dodoma hali iliyosaidia kuondoa
kabisa tatizo la maji katika chuo hicho na katikamanispaa ya Dodoma.
Pia Egwaga
alitoa wito kwa watanzania kutumia huduma zinazotolewa na wakala huo ikiwemo
kufanya utafiti wa maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu,kujenga malambo na
mabwawa,kupima wingi na ubora wa maji yatokayo kwenye visima na ujenzi wa
miradi midogomidogo ya mifumo ya usambazaji maji.
Madhumuni ya
DDCA ni kuongeza kasi ya kutafuta na kuviendeleza vyanzo vya maji kwa gharama
nafuu ili kuboresha huduma ya upatikanaji maji safai na salama na kutosha kwa
matumizi mbalimbali yakiwemo ya majumbani,mashambani, mifugo, ufugaji samaki na
viwandani.
|
0 comments:
Post a Comment