Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Mjini, Jamine Tisekwa akiungana na kwaya ya Kikundi cha
Sanaa za Maonesho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati burudani
ikitolewa bure kwa wananchi katika Bustani ya Nyerere Square mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki. Sanaa JWTZ ilitoa pia burudani za sarakasi,
taarabu, ngoma za asili, Steel Band na muziki wa bendi ya Mwenge Wana
Paselepa
Burudani hiyo
ilikonga nyoyo za wananchi waliofurika kushuhudia ambapo hata muda wa
kumaliza ulipowadia hawakutaka watoke eneo hilo.
Akizungumza
Mkuu wa Wilaya kuhusu onesho hilo, alisema kuwa ni jambo ambalo
hawakulitegemea hivyo wanaomba tena Sanaa JWTZ wapange siku nyingine
waburudishe kuanzia mapema saa nane hadi jioni ili wananchi wa mkoa huo
wafarijike vya kutosha.
Baada ya kumalizi hapo kundi hilo la Sanaa Jwtz lilikwenda kutumbiza usiki kwenye Chuo cha Mipango Dodoma.
Akizungumza
Msemaji wa JWTZ SANAA, Hope Dagaa alisema hivi sasa kikundi chao
wamekiboresha na kwamba hivi sasa wanataka warudi kwa nguvu zote kwenye
kumbi kutoa burudani murwa kwa wananchi, kama ilivyo kuwa zamani.
Mkuu wa Wilaya akicheza pia ngoma ya kibati ya asili ya Zanzibar.
Ngoma ya kibati.
Mwenge Jazz ikifanya vitu vyake.
Wananchi wakishuhudia.
Steel Band ikitumbuiza.
Umati wa wananchi wa Dodoma wakifarijika na burudani murwa iliyokuwa ikitolewa hapo.
Ngoma ya kibati ikichukua nafasi yake.
Mkuu wa Wilaya akiwatuza wasanii.
Msemaji wa Sanaa JWTZ, Hope Dagaa akiwa na Mkuu wa Wilaya Tisekwa.
Mkuu wa Wilaya akicheza wakati kwaya ikitumbuiza.
Mkuu wa Wilaya, Tisekwa akiwa na wasanii wa JWTZ.
Kikundi cha Kwaya.
Steel Band.
Band ya Mwenge Jazz.
Taarab na Sarakasi.
0 comments:
Post a Comment