Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano prof
Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa kampuni za simu nchini zilizo ingia makubaliano na serikali
kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini
kukmilisha kazi hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
Prof.MBARAWA ametoa agizo hilo mkoani IRINGA
mara baada ya kukagua mitambo ya
kampuni ya simu ya TTCL na kubaini kwamba bado kuna baadhi ya vijiji havijafikiwa huduma ya
mawasiliano licha ya mkataba wa
kutekeleza kazi hiyo kati ya serikali na
kampuni hizo kusainiwa miaka miwili iliyopita.
Tulikubaliana kwenye mkataba na tukawapa fedha kwa ajili ya kupeleka mawasiliano
vijijijni hivyo ifikapo mwezi july
kampuni yoyote ya simu itakayokuwa haijatimiza makubaliano hayo tutaipiga
faini, Amesema prof. MABARAWA.
Kuhusu suala la kukatwa kwa mkongo wa taifawa
mawasiliano katika baadhi ya maeneo ya
mkoa wa IRINGA prof.MABAWA amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu
au taasisi itakayoharibu miundombinu
hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL) mkoa wa Iringa Eng. Ekael Manase akitoa taarifa ya Utendaji kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Watendaji wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Iringa.
|
0 comments:
Post a Comment