Serikali
ya Tanzania imewataka wakimbizi wote ambao walikuwa wanajeshi kutoka
nchi walizokuwepo, kuripoti kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa
uangalizi maalum (special protection) kama wanajeshi.
Kauli hiyo ya
serikali imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali
(Mstaafu) Emmanuel Maganga, wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi
duniani yaliyofanyika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma.
Alisisitiza kuwa wakimbizi ambao wako nchini wakijua ni wanajeshi ni lazima wasajiliwe na mamlaka husika.
Aidha Maganga aliwataka vile vile wakimbizi wote ambao wanamiliki silaha wazisalimishe kwa hiari yao wenyewe.
Alisema
kumekuwa na matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na hivyo
kuhatarisha amani na kuwaamuru wenye silaha kuzisalimisha mara moja ili
waende sawa na sheria za nchi walikopata hifadhi.
Maandamano ya
wakimbizi yakiingia uwanjani katika sherehe za maadhimisho ya siku ya
wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu,
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Mkuu huyo wa
mkoa pia alitoa wito kwa mashirika ya misaada duniani kutoa misaada
inayoowana na misaada inayotolewa kwa nchi zilizoendelea na kuongeza
kuwa mahitaji ya binadamu ya msingi hayatofautiani iwe nchi
zilizoendelea au zinazoendelea.
Alisema kuwa
wakimbizi waliopo kwenye nchi zilizoendelea hupewa makazi ya kudumu na
vyakula tofauti tofauti wakati waliopo kwenye nchi zinazoendelea hupewa
mahema na chakula aina moja ambayo ni mahindi.
“Mwaka jana tulishindwa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kuwa tulikuwa tunawapokea wakimbizi kutoka Burundi,” alisema.
Alisema wakimbizi wameongezeka sana nchini na sasa hivi kuna makambi matatu yanayowahifadhi wakimbizi nchini.
Wakati huo
huo Tanzania imepongezwa kwa ukarimu wake kwa kuwahifadhi wakimbizi kwa
zaidi ya miongo minne sio tu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata
duniani.
Mwakilishi
mkazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR , Chansa Kapaya alisema
hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani yenye kauli
mbiu kuwa “Tupo Pamoja na Wakimbizi, Tafadhali ungana nasi”.
“Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mfano mzuri wa kuwahifadhi wakimbizi wengi duniani na pia kuwatafutia suluhu,” alisema.
Mgeni rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga
akizungumza na hadhira iliyokusanyika katika sherehe za maadhimisho ya
siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi
Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Alisema mwaka 2014 Tanzania iliwapa uraia wakimbizi zaidia ya 162,000 baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 40.
Aliongeza kuwa, wakimbizi wanapaswa kuthaminiwa kama binadamu wengine kwa kuwa hakuna mtu anayechagua kuwa mkimbizi.
Kapaya
alisema kuwa kwa sasa kambi ya Nyarugusu ina wakimbizi zaidi ya 131,733
ambao ni wengi zaidi na kusababisha msongamano unaohatarisha maisha yao.
Mwakilishi wa
Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akisoma
risala wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani
yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu,
mkoani Kigoma.
Pichani juu
na chini ni baadhi ya wageni waalikwa, wafanyakazi wa Shirika la UNHCR
na wadau wa maendeleo waliohudhuria sherehe hizo wakifuatilia hotuba
mbalimbali.
Mwakilishi wa
Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akipitia
ratiba ya maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa
yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu. Kulia
kwake ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu,
Emmanuel Maganga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald
Guninita.
Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga (kulia) akifurahi
jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita wakati burudani
mbalimbali zikiendelea kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani
ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani
Kasulu, mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa
Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akiteta
jambo na Ofisa wa UNHCR Tanzania anayeshughulika na mambo ya usalama
kambini, David Mulbah (kulia) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku
ya wakimbizi duniani yaliyobeba kauli mbiu "Tupo Pamoja na wakimbizi.
Tafadhali ungana nasi." ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya
Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Bendi ya
muziki wa Live ya vijana wakimbizi inayojulikana kama Nyota ya Asubuhi
ya kambi ya Nyarugusu ikitoa burudani ya aina yake wakati wa sherehe za
maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Wanamuziki wa bendi ya Nyota ya Asubuhi wakisakata sebene kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Mgeni rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa
Kapaya kwa pamoja wakikabidhi jezi na zawadi kwa timu wakimbizi ya
vijana ya wanawake ya mpira wa miguu katika maadhimisho ya siku ya
wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi
ya wakimbizi Nyarugusu.
Mgeni rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa
Kapaya kwa pamoja wakikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wakimbizi
waliofanya vizuri kwenye masomo yao.
Mkuu wa ofisi
ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu,
Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner akitoa neno la kufunga sherehe za
maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
0 comments:
Post a Comment