SERIKALI imekusudia kutunga
sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya
miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
Hatua hiyo inaelezwa inakusudia
kuinua hadhi ya kazi na ajira za wasichana wa kazi nchini, kwani muda
wa kurasimisha ajira hizo umefikia wakati wake.
Hayo yamebainishwa leo mjini
hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika inayoadhimishwa tarehe 16 Juni
kila mwaka.
alisema hatua inachuliiwa na
Serikali kutokana na wasichana wengi wa ndani kutumikishwa kazi hiyo
katika umri mdogo na kulipwa ujira mdogo.
“Tumepanga kutunga kanuni na
sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya
miaka 18, na ndio maana tunawachukua katika umri mdogo sana na kuwalipa
ujira mdogo, hivyo ukimchukua binti wa miaka 18 utaweza kuinua hadhi ya
kazi ya kazi yenyewe” alisema Waziri Ummy.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho
hayo, Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa kurubuniwa kwa pesa na katika
kuwavichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo
kulawiti na kuwabaka na badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola
ili adhabu kali zichuliwe dhidi yao.
Aidha Waziri Ummy aliwata
wazazi nchini kujenga tabia ya kukagua maumbile ya watoto wao hususani
watoto wa kike ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja kwa mwezi, kwani kwa
kufanya hivyo kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya kimwili ya motto
wake.
Kwa mujibu wa Waziri huyo
alisema vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto wa kike pekee bali na
watoto wa kiume pia wamekuwa wahanga wa vitendo hivyo, ambapo ameitaka
jamii kutowaamini ndugu au jamaa zao kulala kitanda chumba kimoja na
watoto wao.
“Kwa mujibu wa taarifa za jeshi
la Polisi, vitendo hivi vimekuwa vikifanyika zaidi majumbani kwa
asilimia 49, asilimia 23 wakati wa kurudi na kwenda shule na asilimia
15 wakiwa shuleni, hivyo kwa takwimu hizi unaweza kuona ukubwa wa tatizo
ulivyo” alisema Waziri Ummy.
0 comments:
Post a Comment