Mbunge wa
Jimbo la Kilindi, Omari Kigua akiuliza swali kwa Waziri wa Maji na
Umwagiliaji,bungeni Dodoma, ambapo aliihoji serikali kwamba katika
mradi HTM unaotarajia kuwapatia maji Wilaya ya Handeni, kwamba haioni
umuhimu wa mradi huo kwenda pia katika Wilaya ya Kilindi.
Mbunge wa
Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Chatanda akichangia mjadala wa Bajeti ya
Serikali bungeni Dodoma jana, ambapo alimtaka Waziri wa Fedha na Mipango
kukata kodi kwenye mishahara ya viongozi wengine wa juu wa serikali
kama ilivyoamua kukata kwenye kiinua mgongo cha wabunge.
Mbunge wa
Jimbo la Nzega, Hussein Bashe (kushoto), akijadiliana jambo na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwenye viwanja vya
Bunge Dodoma.
Chenge akizungumza na wabunge wa upinzani.
Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige akichangia mjadala bungeni.
Naibu Waziri, Mavunde akijibu maswali ya wabunge bungeni.
Waziri Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Naibu wake, Wambura.
Mary Nagu akiwa na Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa.
Mbunge wa Busokelo, Fred Mwakibete akiuliza swali bungeni kuhusu matatizo ya maji jimboni mwake.
Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (kushoto) akiwa bungeni.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akijibu maswali ya wabunge bungeni.
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali.
Mbunge wa Jimbo la Bariad, Andrew Chengei akijadiliana na wabunge wa upinzani.
Mbunge wa Mtera kichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali.
0 comments:
Post a Comment