Kutokana na baadhi ya watoto kuwa na tabia ambazo hazipendezi watu bila ya kufahamu chanzo chake, imeelezwa kuwa ni vyema wazazi wakajenga mazoea ya kuwafahamu watu ambao wanakuwa karibu na watoto wao ili kuchukua hatua mapema.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia
Nkhoma Ledama wakati wa mahali ya nne ya shule hiyo ambapo watoto wa
ngazi mbalimbali za madarasa walihitimu.
Usia alisema
kuwa wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kujishughulisha na
kazi zao bila kuwa na muda wa kukutana na watoto wao na hivyo kuwa ngumu
kutambua chanzo cha tabia ambazo zinaibuka kwa watoto wao kutokana na
wao kutowafatilia watu ambao wanakuwa karibu na watoto.
"Tunafahamu
wazazi wengi mnakuwa busy na kazi zao na hivyo mtoto akitoka shule
anakuwa na dada au kuangalia tv lakini akiwa katika michezo na watoto
wenzake mnakuwa hamjui ni vitu vya aina gani wanafanya,
"Nadhani ni
vyema sasa kuhakikisha mnawafahamu marafiki wa watoto wenu, marafiki zao
wa shuleni na marafiki zao wa nyumbani, huwezi kujua wanafanya nini
kama huwafahamu tabia watoto wanaocheza nao lakini kama ukiwajua unakuwa
unafahamu rafiki anayefaa ni yupi," alisema Usia.
Aidha
aliwatoa hofu wazazi kuwa shuleni hapo wanawafundisha watoto tabia njema
na wanawafahamu vyema wanafunzi wao hivyo kazi kubakia kwa wazazi
kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wanapokuwa nyumbani.
Mkurugenzi wa
Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama (kushoto)
akizungumza na mmoja wa wazazi Bw. Ally Msoya alipowasili kwenye
mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Msasani
Tower jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa
mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda
Sanga aliwapongeza wanafunzi ambao wamehitimu masomo na wazazi kwa moyo
wao wa kujitoa kuwasomesha watoto wao lakini pia kuwataka kuwasimamia
vyema watoto wao ili waweze kufika mbali kielimu.
"Elimu ni
muhimu sana kwa watoto wenu wanatakiwa kusoma ili kufika mbali kimaisha
niwasihi kuwasimia vyema watoto ili wanapokuwa shuleni wafanye vizuri na
wanaporudi nyumbani pia wafanye vizuri," alisema Eda.
Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mhitimu wa
darasa la Laurey, Thomas Mboya akiongoza watoto wenzake kwenye burudani
maalum wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mwanafunzi wa
Lilies Class, Iptihaj Kinyaga akiongoza darasa la wanafunzi wenzake
kutoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa Laurel Class wakitoa burudani ya kuagana na wanafunzi wenzao katika mahafali ya nne ya shule hiyo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo.
Bwana na Bibi Lugoe wazazi wa mhitimu Abigail Lugoe wakiwa meza kuu.
Wazazi wa
Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitazama burudani na vipaji mbalimbali
vilivyokuzwa shuleni hapo kutoka kwa watoto wao.
0 comments:
Post a Comment