Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 26, 2012


Vitendo vya ukatili kwa baadhi wanawake na utoaji mimba vimendelea kushamili katika nchi yetu ya Tanzania hivi karibuni kumekuwepo kulipotiwa na vyombo vya habari mbalimbali vikilaani vitendo hivyo
Kwamujibu wa Blogg ya Morogoro Yetu Imebaini kuwa vitendo hivyo vimekilithili sana kwa wanafunzi walioko vyuoni kwani hivi karibuni wameokota mimba ya kitoto kichanga chenye jinsia ya kiume kikiwa kimetupwa katika shimo la maji machafu na baada ya kufuatilia ikagundulika kuwa aliye kifanya kitendo hicho ni mwanfunzi wa chuo cha sua mjini Morogoro.
Hata hivyo vitendo hivi vimekuwa vikisikika kwa wingi hata hapa jijini Mbeya.
Wiki mbili hazijapita Amekutwa ametupwa mtoto wa jinsia ya kiume katika ghuba la kutupa takataka katika shule ya msingi mwenge maeneo ya Soweto, Hazijapita siku nyingi katupwa tena motto mwingine. Maeneo hayohayo.
MALAFYALELEO Blogg Inaweza kubaliana kuwa vitendo hivi vimeongezeka jijini Mbeya Labda ni kutokana na kuongezeka kwa vyuo ukweli wa mambo haya utaugundua kuwa limekuwa ni jambo la kawaida kuokotwa vitoto vichanga vikiwa vimetupwa katia mashimo ya vyoo na malanyingine katika baghuba ya takataka.
Hivi ukatili huu utakuwa na majibu gani kwa mwenyezi mungu, Sitaki kuamini kwamba mtu hushika mimba kwa bahati mbaya kama Rugha za wengi hupenda kujitetea, sikubari kushawishiwa na maneno hayo yananitia kichefuchefu We msomi mzima unapanda mbegu usiyo taka kuota na kuivuna inaingia akilini hiyo? Hata hivyo ni kwanini Mnaogopa mimba kulika UKIMWI?
Pumbavu, mjinga wewe Unawezaje kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga? Kwanini mnafanya vitu kama vipofu? Kwanini mnazikosesha haki ya kuishi Roho zisizo na hatia?Kwanini lakini nyie watu mnawaza niniiii jamani mimi ningelikuwa mungu sijui ingekweje?
                           Hasira Imenizidi Tukutane wiki ijayo. 
Mtoto alekutwa ametupwa katika ghuba la Takataka shule ya msingi Mwenge soweto
 

0 comments:

Post a Comment