Zaidi ya
watuhumiwa (88) wametiwa mbaloni na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali
ikiwemo wizi wa kuvunja na kubomoa lakini pia wizi wa mafuta ya magari yanayofanya
shughuri za ujenzi wa barabara ya Tunduma na sumbawanga.
Akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake kamanda Athumani Diwani amesema watuhumiwa
hao wamekamatwa katika msako unaoendelea mkoani mbeya tangu tarehe 08/06/2012
mpaka hivi leo vitu mbalimbali vimekatwa.
Diwani
amesema vitu vilivyo kamatwa ni pamoja na pikipiki tatu (3) Zenye usajiri no
T489 BQU aina ya Sanya T584 BPU aina ya STAR T301 BRU aina ya saug Vitu vingine
ni simu za mkononi,computer laptop, Bunduki mbili aina ya shotgun na Risasi
kumi na mbili Vitu vingine ni Tiv, Radio, nk
Kamanda
Diwani ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kutoa ushirikiano wa kutosha
kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uharifu ili kuliweka mji wetu katika
hali ya usalama zaidi, Lakini pia kwa upande wa wa halifu A mewataka kuacha mara moja kwakua Biashara
hiyo haitalipa tena katika mkoa huu.
Kisha akawataka
wananchi kufika polisi kituo cha kati kwa ajili ya kuweza kuvitambua vitu vyao
iwapo mtu alipotelewa ama kuibiwa kitu.
Kamanda Athuman Diwani akiongea na Waandishi wa Habari Nje ya ofisi yake mkoani.
Kamanda Diwani Akionyesha Bunduki mbili zinazozaniwa kuhusika na vitendo vya uharifu zilizo tengenezwa kienyeji na kutumia risasi za kawaida lakini zinauwa.
Hivi ni Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani mbeya
0 comments:
Post a Comment