WA PILI KUSHOTO MWANEKITI WA KIJIJI CHA MATEBETA BAADHI YA WAASISI WA KIJIJI HICHO |
MWANDISHI WA HABARI RASHIDI MKWINDA AKIONGEA JAMBO KATIKA MKUTANO NA WANA KIJIJI |
MWANDISHI WA HABARI LAUDENCE SIMKONDA AKIMUHOJI MAMA MCHUNGAJI ELIZA SAILENI |
NAMNA YA SALAMU ZA KABILA LA WAMASAI |
WANAWAKE WA KIMASI WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI NA KUPUNGUZA ADHA YA KWENA MWENDO MLEGFU KUPATA MAJI |
MIFUGO IKIFURAHIA KUNYWA MAJI KATIKA MABILIKA YALIYOJENGWA NA WANAKIJIJI |
WAFUGAJI WAKIPATA MAJI SAFI NA SALAMA
Na Laudence Simkonda, Mbeya.
ZAIDI ya Wafugaji elfu Tatu Miatano wa
Jamii ya Kimasai Kijiji cha Matebete wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,
wameamua kuthibiti migogoro ya ardhi ya mara kwa mara na Wakulima kwa
kujiwekea mikakati ya ufugaji wenye tija kwa kupunguza mifugo na
kuweka miundobinu rafiki kwa ajili ya malisho.
Kwa miaka mingi kumekuwepo na migogoro
baina ya wakulima na Wafugaji kugombea maeneo ya Kilimo na Malisho ya mifugo
katika maeneo mengi ya vijiji vya wilaya ya Mbarali ikiwemo kata ya Itambolewo.
.
Matebete ni kijiji kilichopo ndani ya
kata ya Itambolewo, amabacho kwa asilimia tisini kinakaliwa na wafugaji jamii
ya Kimasai.
Wafugaji hao wanadai wamesema wanaeneo la
ardhi lenye ukubwa wa ekari elfu 32,000 ambayo inamilikiwa kwa mjibu wa shereia,
amabyo kwa sasa wanaendelea kuiwekea miundombinu rafiki kwa malisho.
Mwenyekiti wa kijiji Julius Tissho na Mwasisi wa kijiji cha hicho
cha Matebete Mzee Policarp Olekurupashi wamesema kuwa kwanguvu zao wenyewe wafaugaji wa kijiji
cha Matebete, wamaeamua kwenda mbali zaidi kwa kuanza kuweka miundo mbinu ya
maji, ikiwa ni pamoja na kujenga Mabirika kwa ajili ya kunyweshea mifugo yao.
Kutokana na kijiji cha matebete
kukabiliwa nachangamoto kubwa ya ukame, wafugaji wananlazimika kusafiri umbali
mrefu kusaka maji na marisho, hali ambayo inachangia migogoro ya mara kwa mara
baina yao na wakulima, hali ambayo inawafanya kuomba serikali kuunga mkono
juhudi zao.
Kwaupande wake Afisa Mtendaji wa kijiji
ncha Matebete, Sitengas Satullo, amesema kuwa tayari wafugaji wametumia
zaidi ya shilingi milioni 50 katika ujenzi wa Mabirika matatu ya maji, na kudai
kuwa kwa sasa mikakati inayofanywa na serikali ya kijiji ni kuzidi kuboresha
miundombinu hiyo.
Kwa taarifa za Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Kijiji cha Matebete hadi sasa kinamifugo elfu tano, huku akibanisha kuwa
lengo ni kuhakikisha mifugo haitoki nje ya kijiji hicho ili kuondokana kabisa
na migogoro inayo wakumba.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment