Pages

Ads 468x60px

Monday, September 11, 2017

UVCCM waungana na Freeman Mbowe, Waibeza Bavicha Mkasa wa Tundu Lissu


Umoja wa Vijana wa CCM ‘UVCCM’ umelitaka Baraza la Vijana wa CHADEMA ‘BAVICHA’ kuacha kiherehere cha kuingilia taratibu za kiutawala na upelelezi yanapotokea masuala mazito, ikiwemo tukio la kushambuliwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na matukio ya watu kutekwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM (MNEC), Shaka Hamdu Shaka amesema September 9, 2017 aliwasikia BAVICHA kupitia kwa Katibu Mkuu wake wakitoa maneno ya kebehi yanayojenga utata na mkanganyiko akidai yanapalilia chuki na uhasama.

”Matamshi ya BAVICHA yana nia na lengo la kupalilia chuki na hasama kwani yamethubutu kuingilia medani za ki-intelejensia na upelelezi kufuatia tukio la kusikitisha la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na watu wasiojulikana.”
Aidha, amesema kuwa sehemu kubwa katika maelezo ya viongozi wa BAVICHA haikuonyesha ukomavu wala hekima ukilinganisha na ukubwa wa tatizo la kushambuliwa kwa Lissu.

”Tukio la kushambuliwa kwa Lissu si jambo dogo na jepesi kama inavyochukuliwa na BAVICHA, kwani kitendo cha Mwenyekiti na Katibu wake kuishutumu Serikali ni ukosefu wa adabu.”
Shaka amesema yapo matukio mengi ya ujambazi yamewahi kutokea na kupoteza maisha ya watu wakiwemo viongozi wa juu kabla ya tukio la Lissu akilitaja tukio la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Aaman Karume ambaye alipigwa risasi nane kifuani.

”UVCCM kwa mara ya kwanza tunaunga mkono matamshi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliposema huu si wakati wa kunyoosha vidole vya lawama na shutuma huku akivitaka vyombo vya usalama vitimize wajibu wao kiufundi.”

0 comments:

Post a Comment