RC Makalla ahaha, apiga marufuku
Ma-dc, Ma-ded na Wakuu wa Idara kusafiri nje ya Mkoa
Na Moses Ng’wat,Mbeya.
MKUU wa Mbeya, Amos Makalla,
amezuia likizo na safari zote kwa Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara za Mkoa huo,
baada ya kushindwa kuandaa mpango kazi wa kutekeleza dhana
ya Viwanda, ambao ni kipaumbele cha serikali ya awamu ya
Tano.
Alitoa agizo hilo jana Wilayani Rungwe,
wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia na kutoa
majibu ya hoja za Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa hesabu za
serikali (CAG).
Makalla alifikia hatua hiyo, kutokana
na makubaliayaliyofikiwa na viongozi hao June 2 mwaka huu,
ambapo walipeana majukumu ya namna Mkoa huo utakavyotekeleza
uanzishwaji wa viwanda.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema, katika hali
ya kushangaza hadi kufikia sasa hakuna Halmashauri hata moja
ambayo imendaa mpango kazi wa uanzishwaji wa viwanda.
“Kuanzia sasa hakuna, Mkuu wa Wilaya,
Mkurugenzi au Mkuu wa idara kutoka nje ya Mkoa, labda kwa
wale wenye matatizo kama kuumwa na mialiko yote ya semina
sasa isomeni, weka pembeni…maana ukiuliza watendaji
utasikia tuko mbioni, sasa nimeona safari za kufuata mialiko
Dodoma ziwe mwisho. ” alifafanua Makalla.
Aidha, Makalla aliwataka wakurugenzi
wote wa Halmashauri saba za Mkoa huo, wakishirikiana na
Madiwani kusimamia kwa umakini vyanzo vya mapato
ili kuinua mapato na kuepukana na utegemezi kutoka serikali
Kuu.
Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo ya
CAG , Halmashauri hizo za Mkoa wa Mbeya zinajitegemea kwa
asilimia 6.6 tu, huku zikitegemea ngvu ya serikali kuu kwa
asilimia 93.6, kinyume na agizo la Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, aliyeagiza Halmashauri zote nchini kukusanya
asilimia 80 kutoka vyanzo vyake vya ndani.
Akizungumza nje ya kikao hicho, Diwani
wa kata ya Kyimo, Peter Makoye, alipongeza hatua
iliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa akieleza kuwa, limekuja kwa
wakati muafaka kwa kuwa licha ya Rais, Dk. John Magufuli,
kutoa muelekeo wake, bado baadhi ya watendaji wamekuwa
hawatekelez
Naye, Diwani wa kata ya Kawetele,
Anyimike Anganile, alionekana kushtushwa na taarifa
iliyotolewa mbele ya mkuu wa Mkoa kuwa Wilaya ya Rungwe ina
uhaba wa ardhi ya uwekezaj
“Uwezo wa kuwekeza katika viwanda kwa
Rungwe ni mkubwa kwa kuwa, kuna maeneo mengi Mfano kata za
Ilima, Kisondela na Ibigi ambako kuna mashamba ya
halmashauri, lakini shida imekuwa ni dhamira ya viongozi
kutaka kuwekwa mjini” alisema Anganile.
Mkoa wa Mbeya ulikuwa ni miongoni mwa
mikoa iliyokuwa na idadi kubwa ya viwanda, lakini
vilibinafsishwa kwa wakezaji na kushindwa kuviendesha,.
Miongoni mwa viwanda hivyo
vilivyobinafsishwa na kushindwa kuendelea na uendeshajini ni
kiwanda cha nguo cha Mbeya Tixtile, kiwanda cha kutengeneza
zana za kilimo (ZZK), kiwanda cha Sabuni cha Hisoap, pamoja
na kile cha nyama cha Tanganyika Packers.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment