Pages

Ads 468x60px

Monday, September 25, 2017

Bunge lathibitisha Malipo ya Shilingi Milioni 43 Kwenda Hospitali ya Nairobi


Ofisi ya Bunge inapenda kusisitiza kuwa fedha zilizochangwa na Wabunge kiasi cha Tsh. Milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mheshimiwa Tundu Lissu tayari zimetumwa katika Akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu.
Fedha hizo zimetumwa kupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) ambapo kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BOT kwa siku hiyo ilikuwa ni sawa na Shilingi ya Kenya 1,977,120.58.
Kiasi hicho cha Fedha kilitumwa siku ya tarehe 20 Septemba, 2017 kwenda Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham, Akaunti Namba 0451155318 yenye jina la Kenya Hospital Association.
Imetolewa na ; Kitengo cha Habari,
Elimu kwa Umma na Mawasiliano Ofisi ya Bunge DODOMA 24 Septemba 2017

0 comments:

Post a Comment