Pages

Ads 468x60px

Tuesday, October 3, 2017

MAJINA YA WALIOTEULIWA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI WILAYA YA MBEYA MJINI


HATIMAYE Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Mbeya mjini imepata majina ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 5, mwaka huu katika Uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.

Akisoma majina hayo mbele ya viongozi wote waliojaza fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya wilaya hiyo katika ukumbi wa Chama, Katibu wa  CCM Wilaya ya Mbeya mjini  Gellad mwadallu amewataka wagombea wote kuwa na mshikamano na umoja katika kipindi hiki ambacho chama kipo kujijenga upya bila kujali uliteuliwa ama hukuteuliwa.

Kwa wale ambao majina yao hayakuteuliwa Mwadalu amewataka wanachama  hoa kutokata tamaa waendelee kuwa na subira na kuendelea kujenga Chama  kwakua chama hiki ni kikubwa kinazo nafasi nyingi wawe wavumilivu kwa kipindi hiki kwani ipo siku watazipata wakati  ukifika.

Ameongeza kuwa wale ambao  wamepata nafasi ya kuteuliwa basi wajione wanabahati hata kama hawatachaguliwa lakini wameingia katika nafasi muhimu ya kufahamika kwa kusimama mbele ya wanachama zaidi ya elfu moja hiyo tu inatosha kumshukuru Mungu kwani nisehemu pekee ya kuandika historia ya kisiasa.

Aliyataja majina hayo na nafasi zao kuwa ni Ngazi ya Mwenyekiti wa Wilaya kuwa ni pamoja na Affrey Athans Nsomba,Akim Kajigili Mwakalindile na Eden Samwel Katininda huku walioteuliwa kuwania nafasi ya Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi Wilaya ni  Fulco Joseph Mlelwa,Joyasi Godwini Ngajigwa na Philimon Jeremia Mng’ong’o.

Aliwataja wanaowania nafasi ya Mkutano Mkuu wa Mkoa kutoka Wilaya kuwa ni  Atupele Broun Kakyela,  Charles Michael Mwakipesile,  Jackson Waziri Numbi,  Lucy Makelemo Sitta,  Mauld Khamis Issah,  Michaeli Joseph Mbuza,  Nwaka Edson Mwakisu,  Richard Jagjivan Shanghvi,  Seremani Haroubu Said (Mbaspo).

Nafasi ya kuwakilisha Mkutano mkuu wa Mkoa walioteuliwa kugombea ni  Godrey Kapunga Habaya,  Isaack Samson Sintufya,  Jackson Waziri Numbi,  Joyce Paul Stambul,  Maria Dominiki Nyagawa,  Suzana mwalwanda Simkoko na  Tumwitike Nsubili Sanga.

Aidha alizitaja nafasi za Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya kuwa ni  Abdalla iddi kilanga, Aleni Joseph Mbuza, Angetile Amisi Kipimbilo, Charles Michael Mwakipesile, Damasi tuyanje Manjela, Edith Peter Kapwela, Fortunatus Bethod Tapule na Francis Mwambopo Mwangoke.

Wengine ni  Godrey Kapunga Habaya, Innocent Sadoki Kimambo, Isaack Samson Sintufya, Joackomu wilson Motella, Joel alon mhanga, Lydia John Gunda, Paulo Lukckson Shikungu, Malanyingi Ahmed Matukuta, Maria Dominiki Nyagawa na Mauld Khamis Issah.

Wakiwa pamoja na Mary Elia Mwaijumba, Martin Boniface Mponzi, Maryprisca Winfried Mahundi, Michael Joseph Mbuza, Patric Toi Kahesh, Philimoni Jeremia Mng’ong’o, Richard Jogjivan Shanghvi, Seramani Haroub Said (Mbaspo), Shabani Juma Chalo, Thomas Aseri Mwanga, Tumwitikege Nsubiri Sanga na Vincent Mahudi Msolla.

RICHARD JONGVAN MMOJA WA WAGOMBE AKICHANGIA MADA KATIKA KKIKAO CHA WAGOMBEA
KATIBU WA VIJANA JERRAD KINAWILO KUSHOTO NA KATIBU WA UWT MARY MWENISONGOLE KATIKATI WAKISIKILIZA KWA MAKINI KATIKA KIKAO CHA WAGOMBEA







WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI KATIKA KIKAO CHA KUSOMEWA MAJINA YA WALIOTEULIWA.

0 comments:

Post a Comment