Thursday, March 26, 2015

Breaking News:- Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi majengo amekutwa amekufa ndani ya shimo la maji machafu lililopo mita chache na nyumba yao.baadhi ya mashuhuda wagubikwa na utata wakifo chake baada ya kumkuta akiwa amefungwa kamba mguuni mwake na mikwaruzo usoni  pia akiwa hana nguo  za ndani.


 
 Mwili wa mwananafunzi Asia mwandenga muda mchache baada ya kutoa kutoka katika shimo la maji machafu
                        Shimo la maji taka ambalo umekutwa mwali wa mwanafunzi Asia mwandeanga

Mama mzazi wa mwanafunzi akiwa ameshikiliwa akilia kwa uchungu baada ya polisi kufika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa mwananfunzi.


Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa mwanafunzi kisha kuondoka nae kwa uchunguzi zaidi kwahabari zaidi  juu ya tukio hili fuatilia katika ukurasa huu.

Askofu wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi Alinikisa Cheyo amewetaka viongozi wa kanisa kuwajibika katika kazi.Hayo yamebainishwa  leo wakati  akizungumza na mwandishi wa habari hii katika semina ya siku nne iliyoandaliwa na kanisa hilo  inayofanyika katika ofisi za kanisa hilo zilizopo Jakaranda jijini Mbeya.
Askofu Alinikisa Cheyo(picha na maktaba yetu)


Amesema swala la uwajibikaji kwa watendaji wa kanisa  limekua tatizo kubwa ambalo limepelekea kuwepo kwa semina za mara kwa mara kwa wakuu hao ili kuwajengea uwezo katika utendaji  wa kazi zao za kila siku.
                                        
“Watumishi wengi  wamekuwa wakichaguliwa na Halmashauri kuu ya kanisa bila kujua wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao mara nyingi hujikuta wanafanya kazi wakisukumwa na roho mtakatifu tofauti na viongozi wanaotoka Serikalini hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko hawa” amesema Askofu Cheyo

Nae Zacharia Sichone Makamu mwenyekiti wa kanisa hilo amesema wameamua kuendesha semina hiyo ili kuwajengea uwezo viongozi hao kwa lengo la kuwaimarisha na kuona wanajua wajibu wao ili wakishindwa kutekeleza majukumu yao basi wajihukumu wao wenyewa kukushindwa kutekeleza kinacho wapasa kufanya.

“Tunaweza kulaumiana na kwa makosa mbalimbali kwa wakati mwingine si kwa makosa ya watu kumbe nikutokana na uelewa mdogo walio nao hawajui wajibu wao, Kupitia mafunzo haya kila mmoja atajua kinacho mpasa kufanya na kisha kufikia malengo makubwa na kuleta maendeleo katika kanisa letu” Amesema Sichone.

Kwa upande wake Agripa Senka mkurugenzi wa uchumi, mipango na maendeleo amesema kumekuwepo na mpango wa miaka minne ya kuendesha mafunzo ya namna hiyo  kwa  hivyo kwani viongozi wengi huchaguliwa bila kuwa na maarifa ya uongozi kupitia semina hizo zitafanya viongozi  kuwa na uwezo wa kiutendaji na kujiamini katika kazi zao.

Pia Nyandu Kajange katibu wa wilaya ya chunya ambae ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo amesema wamejifunza kusimama vizuri katika nafasi zao nakupanga mipango  ya kazi nyenye utekelezaji mzuri na  kujiamini katika uongozi na kuleta maendelao katika taasisi husika.
                                               mwisho 
 Katibu mkuu wa kanisa la moraviani Tanzania mmoja wa wakufunzi wa semina akiongea jambo wa wanasemina

 Viongozi na wakuu wa taasisi za kanisa la moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi wakisikiliz za kwa makini mafunzo yanayoendelea
          Makamu wa mwenyekiti Zacharia Sichone akijangia moja ya mada katika Semina hiyo
                Devule mwambije mkaguzi wa ndani wa kanisa akongea kitu katika semina

                                                                            Mwisho


Wednesday, March 25, 2015

RISASI ZARINDIMA DAR ES SALAAM - TENA, MAJAMBAZI WAWILI KUTOKA ITALI WAKIONA CHA MOTO - TUKIO KATIKA PICHA

 
Habari zinasema kuwa polisi mkoani dar es salaam jana mchana walifanikiwa kuwatia mbaroni majambazi wawili ambao inasemekana ni raia wa italia baada ya kupora kiasi cha dola elfu kumi kwa mwananchi ndipo polisi walipoanza mapambano nao na hadi kuwatia nguvuni baada ya luwadhibiti na risasi. PICHA ZOTE KWA MSAADA WA http://jijiletublog.blogspot.com/


Monday, March 23, 2015

Mamlaka ya Majitaka na Majisafi ya jijini Mbeya yakili kuwepo kwa tatizo la chemba ya majitaka inayo tililisha maji katika mto wa Dauseni jijini Mbeya kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.Mamlaka Imeahidi kuijenga chemba hiyo haraka iwezekanavyo ili kuwapunguzia wakazi wa kata ya majengo kero hiyo ndani ya wiki mbili zijazo ili kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ya milipuko.

Baada ya kilio cha muda mrefu sasa kwa wakazi wa jiji la Mbeya kata ya majengo kwa kile walichodai kero ya chemba ya majitaka kutililisha maji hayo katika mto wao unaotumika na idadi kubwa ya wakazi hao kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kuhatarisha afya zao na kuahidi kuijenga chemba hiyo ndani ya wiki mbili.

Akiongea na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake mkurugenzi mtendji wa mamlaka ya majisafi na majitaka Eng: Simion Shauri amesema hakuwa na taarifa ya tatizo hilo hivyo amewataka wakazi hao kuwa na subira kwani suala hilo litashughulikiwa haraka iwezekanavyo.
 
Eng: Simion Shauri akiongea na wakazi wa majengo,  

“Nawaomba wakazi wa majengo kuwa wavumilivu kwa tatizo walilonalo litatuliwa ndani ya wiki mbili zijazo na kuwafanya waishi kwa amani kama kawaida, ni kweli sikuwa na taarifa ya tatizo hilo la sivyo lingekua tayari limetatuliwa kwa muda muafaka na kuiondoa kero hiyo kwa wakazi ambao wamekua wakilalamika”amesema Shauri.

Ameongeza kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi ili kujiunga na huduma ya mtandao wa uondoshwaji wa majitaka kutoka katika majengo yao na kwa sasa mamlaka imeondoa gharama za kuunganishwa katika mtandao huo na kuwapa mabomba mita 30 bure wateja wake ili kuhamasisha na kuwapa unafuu wa huduma hiyo.
Naye Eng: Mloelya Paul amesema tatizo hilo lilisababishwa na ujenzi wa barabara uliokuwa ukifanywa na Halmashauri ya jiji la Mbeya na kubomoa chemba hiyo na kuziba na hivyo kufanya shughili ya kuizibua kuwa ngumu kwa kua ilizibwa na mawe makubwa ambayo yanatakiwa kuchimbwa ili kuyatoa.
Eng: Mloelya Paul akisoma Risala kwa mgeni rasmi

 “tatizo hilo lipo kwa muda mrefu sasa tulikuwatunashughulikia bajeti yake ambayo mpaka sasa imekamilika ndani ya wiki hii tutaanza kulichughulikia na ndani ya muda wa wiki mbli zijazo litakua limekamilika wakazi hao wategemee kuondokana na kelo hiyo iliyosababishwa ujenzi wa barabara za halmashuri ya jiji ambao hubomoa miuondo mbinu hiyo mwanapoendesha shughuru zao hizo” amesema Mloelya.

Hatua hiyo imekuja baada ya kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa kata ya majengo ambao walikumbwa na mshangao mkubwa baada ya mamlaka hiyo kujenga chemba mpya kwa muda wa masaa 24 na kuizindua katika  maadhimisho ya wiki ya maji na kuicha chembe iliyokua kero kubwa kwao iliyopigiwa kelele kwa muda mrefu na kutopatiwa ufumbuzi,

    Chemba ya majitaka inayotililisha majitaka katika mto Dauseni ambayo ni kero kubwa kwa wakazi wa kata ya majengo

Mto huo maji yake hutumika kwa matumizi mbalimbali kama mwandishi wa habari hii alivyo wakuta wanafunzi wa shule ya Sekondali ya Rejiko wakichota maji hayo yenyekuchanganyikana na majitaka

Saturday, March 21, 2015

Sirikisho la vyuo vikuu mkoani Mbeya wamtaka Prof: MARCK MWANDOSYA kujitokeza kuwania uraisi uchaguzi mkuu ujao.


Hayo yamejili katika kongamano la wasomi hao lililohusu uchaguzi  mkuu wa mwaka 2015 na kuonesha nia yao ya kumshawishi kugombea nafasi hiyo.
 IDD MAMBO KATIBU ITIKADI NA UENEZI CHUO KIKUU TEKU AKIMKARIBISHA MSEMAJI WA TAMKO HILO.

 BAADHI YA WANACHAMA WA CCM NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WALIOKUWEPO KATIKA KUTOA TAMKO HILO

 OSCAR MWAIHABI KATIBU WA SHIRIKISHO LA WANAZUONI AKITOA TAMKO KWA NIABA YA WANAZUONI MKOANI MBEYA KWA WAANDISHI WA HABARI


Soma hapa:

Na: Charle Abraham


Sirikisho la vyuo vikuu  mkoani Mbeya wamtaka Prof: MARCK MWANDOSYA kujitokeza kuwania uraisi uchaguzi mkuu ujao.

Hayo yamejili katika kongamano la wasomi hao lililohusu uchaguzi  mkuu wa mwaka 2015 na kuonesha nia yao ya kumshawishi kugombea nafasi hiyo

 Katika siku za karibuni kumekuwapo mjadala mkubwa ndani ya CCM juu ya mtu atakayepitishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, na ilizidi baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa mwanachama ambaye atateuliwa na CCM kugombea urais hayumo miongoni mwa waliojitokeza na kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze


 Wakati joto la urais likizidi kupanda ndani ya CCM kutokana na hofu ya baadhi ya majina mazito ya wagombea wa nafasi hiyo kuendelea kujitokeza na ikiwa ni pamoja na kujinadi kwa sili hali hiyo imechukua hatua zaidi baada ya shirikisho la vyuo vikuu mkoani Mbeya kufaya kongomano la uchaguzi mkuu  lililofanyika katika ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini hapa nakuchukua nafasi hiyo ya kumshawishi Prof: MARCK MWANDOSYA kugombea nafasi ya uraisi.

Akisoma tamko loa wanazuoni hao mbele ya waandishi wa habari katibu wa shirikisho hilo OSCAR MWAIHABI toka chuo kikuu cha tumaini amesema wamefikia uwamuzi huo baada ya kuona ndani ya chama hicho hakuna kiongozi mwenye sifa ya kufanana nae na hivyo wangeona Tanzania ijayo ikiongozwa na kiongozi huyo.

“Sisi wanazuoni tumeona kuwa wewe Prof: MARK  J. MWANDOSYA unafaa kabisa kupokea kijiti cha uraisi kutoka kwa JAKAYA KIKWETE kwakua unafaa ni tofauti na wengine wote waliojitokeza kutangaza nia katika Chama Cha mapinduzi kutokana nauongozi ulio wahi kushiriki kuongoza hujawahi kupata tuhuma yoyote mpaka leo hii, pia Taifa linahitaji kiongozi mwenye hekima na maamuzi magumu hata utafiti unaonesha uwezo ulionao wa kiuongozi” amesema Mwaihabi

Ameongeza kua Mwandosya ni mengi mazuri ameyafanya katika uongozi wake ndani ya Taifa hili, Hivyo wao kama wanazuoni wanamuomba kwa heshima kubwa ashawishike kugombea nafasi hii adhimu katika Taifa hili ya Uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama Cha mapinduzi kama Dr. Jakaya Kikwete alivyo wataka wanachama wa CCM kuwashawishi watu wenye uwezo ambao hawajajitokeza kutangaza nia zao wajitokeze. 

Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni waziri wa Maliasili na Utalii.

Lakini pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita, William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na Edward Lowassa ambaye ameibua mjadala kati ya kambi yake na zinazompinga.
                                                                              Mwisho