Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua majengo ya maabara za shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari
ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala, Leo 2 Aprili 2018.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakifatilia mkutano wa hadhara ukiongozwa na Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani
Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko akikagua ujenzi wa nyumba za madaktari wa kituo cha
afya cha Uyovu akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka
Biteko Leo 2 Aprili 2018 amechangia matofali 10,000 kwa ajili ya
ukamilishaji Wa vyumba vya maabara ili kurahisisha uanzisha Wa shule ya
sekondari Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe.
Shule ya sekondari
Busonzo inahitaji kukamilisha maabara tatu ili iweze kufunguliwa ambapo
serikali imetoa milioni 40 kwa ajili ya kazi hiyo.
Mhe Biteko amechangia
matofali hayo Mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa
aliyoyatoa wakati Wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa
mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita kwa kuwataka viongozi wa
mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro
wa wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari wahamasishe umuhimu wa
elimu na mahudhurio endelevu shuleni.
"Mkoa wetu tumepata
aibu kubwa kwa kuwa namba mbili kwa utoro kati ya mikoa yote nchini,
utoro huu hapa wilayani kwetu unachangiwa na umbali wa kwenda shuleni,
hapa Busonzo watoto wetu wanasoma Runzewe ambapo ni mbali sana. Umbali
huo unachangia utoro" alisisitiza Mhe. Biteko
Katika sherehe hizo
zilizonakshiwa na Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ambayo ni
‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
Waziri Mkuu alisema kuwa utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni mkubwa zaidi
kwa Mikoa husika kuliko shule za msingi.
Mara baada ya uzinduzi
Wa Mwenge huo wa Uhuru kabla ya kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya
shughuli za Bunge zinazotarajiwa kuanza kesho 3 Aprili 2018 Mhe Doto
Biteko amezuru Kijiji cha Nampalahala kilichopo Kata ya Busonzo na
kujionea jinsi ujenzi Wa maabara unavyoendelea.
Mara baada ya kubaini
kuwa kuna upungufu wa matofali 10,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi
huo, Naibu Waziri huyo amechagiza ujenzi huo kwa kuchangia gharama za
ununuzi wa matofali hayo ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.
"Mheshimiwa Waziri
Mkuu ameshatoa maelekezo ya kukomesha utoro naomba tukimbie kulitekeleza
hilo na ninaomba wazazi tuhakikishe watoto wote wanakuwa shuleni ni
aibu mno sisi kuwa vinara wa utoro". Aliongeza Mhe. Mbunge Na Naibu
Waziri huyo.
Mhe Biteko amewaeleza
wananchi hao jinsi ambavyo utoro kwa shule za sekondari Mkoani Geita
umekithiri jambo ambalo limepelekea Mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa
utoro Kitaifa kwa asilimia 8.1, ambapo Mtwara imekuwa nafasi ya tatu kwa
asilimia 6.4, Shinyanga asilimia 6.3 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa
na Mkoa Wa Tabora kwa asilimia 9.7
Aidha, Mhe Biteko
ameonyesha kusikitishwa na takwimu za Mkoa Wa Geita kushika nafasi ya
pili pia katika kwa utoro kwa shule za msingi kwa kwa asilimia 3.1 nyuma
ya Mkoa Wa Rukwa unaoongoza kwa asilimia 3.2
√ Do Cong Ty Co Phan On Ap Bien Ap Standa Viet Nam san xuat
ReplyDelete√ Tren may Standa co tem cao SMS chong hang gia hang nhai
√ Vo may Standa so tinh dien dac biet
√ Dinh may Standa duoc dap chim chu standa
Quy khach co the chon may cong suat lon hon nhu Standa 15KVA Lioa Standa 20KVA theo nhu cau
☎️ Hotline 0915 951 325 de co gia standa tot hon
On ap; bien ap Standa chuan day dong 100%; Phan phoi on ap lioa gia tot nhat.