ILI kuondokana na tabia ya utegemezi kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia, wametakiwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kujiajiri kwenye uwakala wa bima za vyombo vya moto.
Aidha imeelezwa kuwa kupitia
vikundi hivyo wanaweza kuanzisha makampuni ya Uwakala wa Bima na kuweza
kuendesha biashara kama watu wengine na hatimaye kujipatia vipato.
Hayo yamesmwa na Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Nyanda za juu kusini, Consolata Gabone katika semina ya walemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha ufundi
( VETA ) jijini Mbeya.
Meneja huyo amesema Watu wenye
ulemavu wa kutosikia wanaweza kujipatia
kipato cha kujikimu kimaisha na kuondokana na uchumi tegemezi kwa jamii
inayo wazunguka.
Amesema semina hiyo yenye lengo
la kufundisha umuhimu wa Bima kwa jamii ili kuepuka na namna kukabiliana na
majanga ya ajali ya vyombo vya moto.
Consolata amesema mamlaka inao wajibu wa kusajili wadau wa
bima, makampuni, mawakala na wakadilishaji wa Hasara ikiwa ni pamoja na kukagua
makampuni ya Bima madalali na mawakala pia kushughulikia malalmiko ya bima
kutoka kwa wakata bima na jamii kwa ujumla kazi ambayo inaweza kufanywa na mtu
yeyote bila kujali hali aliyonayo.
”Nawakaribisha kujiunga katika
vikundi ili muweze kuanzisha makampuni na kuja kwetu mamlaka ya usimamizi wa
Bima ili tuwasajili na kisha kuanzisha biashara ya uwakala na kujipatia ajira
itakayo wapatia kipato kitakacho wakimu katika maisha na kuondokana na
utegemezi” Amesema Consolata.
Nae Afisa shirika la bima la (
NIC) jijini hapa, Michael Msata amewataka walemavu hao kuwa na elimu ya bima
na kukata bima katika shughuli zao mbalimbali ikiwa ni
pamoja na bima ya mali, nyumba, ajali, Afya na nyumba, ili kuepuka hasara endapo kutatokea
hasara.
Kwa upande Kaimu Mwenyekiti wa
Chama cha watu wenye ulemavu wa kutokusikia Mkoa wa Mbeya (CHAVITA) Tusajigwe
Mwalwega ameupongeza uongozi huo kwa kutoa semina hiyo kwa makundi maalumu kwani
wengi hawajui maana ya bima na kwamba ni kitu cha muhimu katika maisha ya kila
mwanadamu.
0 comments:
Post a Comment