Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)
wilaya ya mbeya mjini Gerralad Mwadallu amewataka viongozi waliochaguliwa
kutoka katika nfasi ya utendaji, Makatibu wa matawi na kata zote wilaya mbeya
mjini kua viongozi wenye maadili kwa jamii.
Ameyasema hayo katika Semina ya
siku moja kwa viongozi hao iliyo andaliwa na ofisi za CCM wilaya ya mbeya mjini
yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao, semina imefanyika katika ukumbi
wa shule ya sekondari Sangu jijini Mbeya.
”Siku ya leo tumeona ni vema
kukutana na viongozi wote watendaji ili kuelezana namna ya utendaji ndani ya
chama chetu tumewaita watendaji tu ili mjue wajibu katika utekelezaji wa
majukumu yenu, Kwakua chama hiki ni kipya hakitaki mtu ambae hayupo tayaki kuwa
mchapa kazi kama kuna mtu kaingia kwa bahati mbaya atupishe hatuna utani katika
hili” amesema Mwadallu
Ameongeza kua kiongozi
anaetakiwa kipindi hiki ni Yule mwenye uelewa juu ya kupambanua mambo,mwenye
mwenendo na tabia njema kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuwajibika mbele ya umma
na kua na kauli nzuri kwa anaowaongoza.
Nae Charles Mwakipesile mjumbe
wa kamati ya siasa wilaya ya mbeya mjini alisema wapo watu ambao wamekuwa
wakibeza utendaji kazi wa Dk. Magufuli na kwamba kazi hiyo ni sehemu ya
Propaganda hivyo Wanaccm wanapaswa kusimama kidete katika kutoa elimu na
kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Aliongeza kuwa wapinzani
wamekosa sera za kuwaeleza wafuasi wao badala yake wamejikita katika kuelezea
propaganda ambayo lengo lake ni kupotosha na kuelezea uuma na kuaminisha kuhusu
uongo jambo linalopelekea kuishia kulalamika kila siku.
Kwa upande wake Katibu wa
Wazazi Wilaya ya Mbeya mjini, Sadick Kadulo alisema ili Chama cha Mapinduzi
kiendelee kushika dola kwa miaka mingi zaidi lazima kiwe kinafanyiwa mabadiliko
na marekebisho ya mara kwa mara ili kuboresha kuendana na wakati.
Nao baadhi ya washiriki wa
mafunzo hayo waliupongeza uongozi wa CCM Mbeya mjini kwa kuwajali na kuwapa
mafunzo na kuongeza kuwa huko nyuma walikuwa wakiongoza kwa kutumia utashi wao
na sio kupatiwa semina kama hiyo.
Mwisho.
VINONGOZI WA KAMATI YA SIASA MBEYA MIJINI NA MJUMBE CHARES MWAKIPESILE AKIONGEA JAMBO KATIKA SEMINA HIYO
KATIBU WA VIJANA WILAYA YA MBEYA MJINI (UVCCM) GERRALD KINAWILO AKIONGEA JAMBO
Katibu wa Wazazi Wilaya ya Mbeya mjini, Sadick Kadulo mmoja wa wakufunzi wa semina hiyo akiongea.
Katibu wa Wazazi Wilaya ya Mbeya mjini, Sadick Kadulo mmoja wa wakufunzi wa semina hiyo akiongea.
0 comments:
Post a Comment