Imesema
hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa
misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za
uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi
ametangaza uamuzi huo leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari.
Dk Abassi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017.
Amesema
kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo
juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.
Amezitaja
baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa
Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari "Ufisadi ndani ya Ofisi ya
JPM".
Dk
Abassi amesema, "Habari hii ilisheheni nia ovu dhidi ya Rais wakati
suala husika lilihusu Shirika la Elimu Kibaha, wahariri walikiri udhaifu
wakaomba radhi na kupewa onyo kali."
"Tulipowaita
wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno
yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa
habari lazima izingatie maadili," amesema.
0 comments:
Post a Comment