Ndege
ndogo ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyombeba Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ikiwasili
katika uwanja wa ndege wa Mpanda ,Meja Jenerali Milanzi anatarajia
kufunga rasmi Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari
waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika katika
Kambi ya Mlele iliyopo Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenrali Gaudance Milanzi
akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa
nchini (TANAPA) Allan Kijazi alipowasili katika uwanja wa ndege wa
Mpanda mkoani mkoani Katavi kwa ajili ya shughuli ya kufunga Mafunzo
hayo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) Allan Kijazi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpanda.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi
akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za
Taifa nchini (TANAPA) Mtango Mtahiko.
Mkurugeni
wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) akimuongoza Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi
,kuelekea chumba cha mapokezi cha watu mashuhuri katika uwanja wa ndege
wa Mpanda mkoani Katavi.
Watendaji
wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) wakiongozwa na Meneja
Mawasiliano wa Shirika hilo Pascal Shelutete wakiwa katika mkoa wa
Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyeko mkoani Katavi.
0 comments:
Post a Comment