eGA
yataka Taasisi Mbalimbali kutekeleza Miradi ya TEHAMA.
Na: Frank Shija, MAELEZO
02/06/2016
Ofisi naTaasisi za umma zashauriwa kushirikiana naWakala
wa Serikali Mtandao (eGA) katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya
Tehama.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano
wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)
Bibi. Suzan Mshakangoto wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam.
Bi. Mshakangoto amebainisha kuwa kumekuwapo na changamoto
ya Taasisi za umma kuanzisha miradi ya TEHAMA inayofanana huku zikiwa na taarifa
zinazokinzana na kuisababishia gharama zisizo za lazima Serikali.
Aidha alisema kuwa ili kujiridhisha na miradi ya
TEHAMA Wakala hiyo imeweka vigezo katika Orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA Serikalini,
inayopatikana katika tovuti ya Wakala ili uweze kuhakikiwa na kuthibitishwa.
“Kutokana na utaratibu huo kuleta changamoto mbalimbali,taasisi
yeyote ya umma inatakiwa kuwasilisha mradi wake kwaWakalaya Serikali Mtandao ukiwa
unaendana na vigezo vilivyowekwa katika orodha ya miradi ya
TEHAMA Serikalini inayopatikana katika tovuti ya wakala ambayo ni www.ega.go.tz”
AlisemaBi. Suzan.
Changamoto zinazojitokeza kutokana na utaratibu huo ni
pamoja na kutofautiana kwa taarifa ya aina moja kutoka taasisi tofauti akitolea
mfano wa Rita wanaweza kuwa na Jina la Juma Hassan na mtu yulelyule ukienda Bima
ya Afya anaitwa Juma Kassim Hassan.
Kutokana na mkanganyiko huo na Wakala inashauri na kuzitaka
taasisi zote za Serikali kuwasilisha andiko la miradi yao ya Tehama kwa Wakala ya
Serikali Mtandao ili kuhakikiwa kama zinakidhi vigezo, malengo na dira ya maendeleo
ya Serikali ya mwaka 2025 na kama mradi huo niendelevu.
Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha
na miradi au utengenezaji wa mifumo ya Tehama Serikalini kujiridhisha kama miradi
waliyokusudi kuitekeleza inakidhi vigezo vya kuanzisha miradi ya TEHAMA kama vilivyoainishwa
katika orodha ya miradi ya Tehama Serikalini.
Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) ni taasisi ya Serikali
kwa mamlaka iliyonayo kisheria inawajibika kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu
Serikali Mtandao hivyo ni wajibu wake inapoona mambo yanaenda kinyume na taratibu
na miongozo ya usimamizi wa miradi ya Tehama Serikalini.
0 comments:
Post a Comment