Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Askofu
wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku
tatu walioficha sukari kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi
iwakatae.
Askofu
Gadi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari juu ya uhaba wa sukari nchini na maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.
“Tanzania
haina tatizo la sukari bali sukari ziko kwenye maghala, wafanyabiashara
wamezificha ili waje kuuza kwa bei ya juu. Tunamuomba Mungu ili watu
hao ardhi iwakatae ikiwa hawatatoa sukari ndani ya siku ya tatu,”alisema
Askofu huyo.
Pia,
Askofu Gadi ametoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha
sukari na wakumbuke kuwa waislam wapo katika maandalizi ya kutimiza
nguzo muhimu ya imani ya dini yao ambapo wataanza mwezi wa Ramadhani na watahitaji sukari kwa ajili ya kuandaa futari.
Vile
vile Askofu huyo ameiomba Serikali kuagiza sukari kwa wingi ili waumini
wa dini ya Kiislam waweze kutimiza kwa urahisi nguzo ya mwezi wa
Ramadhani.
Aidha,
akizungumzia juu ya mkutano wa maombi utakaofanyika jiji la Arusha,
Askofu Gadi amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kumuombe
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kufanikiwa katika nia yake ya
kujenga upya uchumi, uadilifu na ustawi wa Tanzania.
Mkutano
huo unategemewa kufanyika siku ya Jumatano Juni 08, 2016 kuanzia 4
asubuhi mpaka saa 12 jioni viwanja vya relini, ambao umeandaliwa na
Kanisa la Good News for All Ministry kwa kushirikiana na Umoja wa
Makanisa ya Arusha.
0 comments:
Post a Comment