Pages

Ads 468x60px

Sunday, June 30, 2013

ANGALIA PICHA RAIS BARACK OBAMA ALIVYOPOKELEWA NA WAANDAMANAJI AFRIKA KUSINI.


Akiwa na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma kulia kwao ni wake zao.
Waandamanaji wakiwa tayali kuanza maandamano ya Amani.
HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA VIUNGA VYA MKI WA CAPE TOWN.

Moja la bango la waandamanaji likiwa chini.
Kama unavyojionea mwenyewe.
kazi kweli kweli.
Wakiyaandaa mabango .

Uku ikiwa wanakumbuka kwamba kiongozi wao wa kwanza Mweusi Mzee Nelson Mandela yuko Hospitali akiendelea kupata matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya Baadhi ya wananchi wa Afrika kusini walijitokeza nje ya ukumbi wa Bunge mjini Cape Town kuandamana kupinga ziara ya Rais wa Marekeni Obama,uku wakiwa na Mabango yenye kuonyesha ujumbe mbalimbali kwa rais huyo

 

Waandamanaji Nchini Afrika Kusini, Wakisali mbele ya Bango linalopinga ziara ya Raisi Obama nchini humo, Afrika Kusini
WAKATI Rais wa Marekani Barack Obama akianza ziara yake nchini Afrika Kusini,baada ya kutoka Senegal kabla ya kufika nchini Tanzania,wananchi wa Afrika Kusini jana walimpokea Rais huyo kwa maandamano na mabango.
Maandamano hayo ya amani yaliandaliwa na kikundi cha waumini wa dini ya Kiislamu nchini humo na kuishia katika ofisi za Ubaloziwa Marekani, mada kubwa katika mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao ni kuhusu mauaji na vita vilivyo endeshwa na Marekani katika baadhi ya nchi za Kiislamu.
Waandamani hao walidai kwamba, Rais Obama na nchi yake ndiyo vinara wa vita nchini Iraq,Vietinam na baadhi ya nchi zingie za Kiislamu ambazo walidai kwamba ziliingia vitani kwa sababu za propaganda za Marekani.

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28

 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP

JK AWAANDALIA DHIFA YA CHAKULA CHA USIKU MARAIS DAR


 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.

 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
 Msanii Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge hilo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
                                              Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera

Saturday, June 29, 2013

RAIS KIKWETE AFANYA UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP JIJINI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
Rais Omar Bongo katika mjadala huo
Kijana akichangia
Vijana wakichangia mjadala
 
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala
 
Kijana akichangia katika mjadala
Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala
 
 
 
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
Wageni mbalimbali katika mkutano huo
Ujumbe wa Swaziland
Ujumbe wa Tanzania
Meza kuu
Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza
 
 
Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha
 
Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni