Pages

Ads 468x60px

Monday, May 7, 2012


    

MBUNGE MARY MWANJELWA AKANUSHA  KUHAMA CCM


 Mbunge wa viti maalum mbeya mjini kupitia chama cha mapinduzi ccm MARY MWANJELWA amekanusha uvumi ulioenezwa na chombo kimoja cha habari kuwa anategemea kukihama chake cha ccm na kuenda chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Kwa kile alichodai kuwa Rais amewachagua wabunge wageni na kuwapa uwaziri hivyo kuwa dhalilisha wale wa zamani.
Hayo ameyasema leo katika kikao chake na wandishi wa habari kilichofanyika katika ukumbi wa ccm mkoa, nakuongeza kuwa  hana mpango wala hategemei kukihama chama chake hicho kwani yeye amechaguliwa kutetea wananchi wa mbeya hivyo hawezi kuwasaliti.
 Hata hivyo amesema ataendelea na ubunge kwa muda wote uliosalia wa miaka mitatu kwani mpaka sasa amewatumikia wananchi wake  kwa muda wa miaka miwili tu hivyo anategemea kugombea tena muhura ujao wa uchaguzi ili kutetea kiti chake.
 Kikao hicho kimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi ccm akiwepo katibu HERENA SHIMBUSHO, Katibu umoja wa wananwake(UWT) mkoa TABU LUNGWESA, katibu wilaya ya mbeya mjini RAYMOND SITIVINI pamoja na katibu mwenezi mkoa BASHIRU MADODI.

 Waandishi wa habari wakimsikiliza MARY MWANJELWA Akikanusha kukihama chama chake cha ccm.

0 comments:

Post a Comment