Watanzania
wenge wamekuwa na kasumba mbaya yakutokuona umuhimu wa mikutano ya vitongoji,
vjiji na mitaa hivyo kupelekea kushindwa kuwakilisha karo na mataatizo yao na kuona viongozi
waliowachagua kuwa ni watendaji wabovu na wasiowajibika kwao
Hayo
yamesemwa na diwani wa kata ya Inyala MWALINGO M. KISEMBA katika mdahalo
ulioandaliwa na mtandao wa asasi za kiraia mkoani mbeya (MBENGONET) kwa malengo ya kuimalisha mahusiano na kuongeza wigo wa majadiliano
kati ya wabunge, madiwani na wananchi
“Jukumu la diwani
ni kuchukua matatizo na kero za wananchi na kuipelekea serikali, Pia kuhamasisha
wananchi katika shughuri za maendeleo na kuwawakilisha wananchi katika baraza
la madiwani katika halmashauri nakushiliki kupanga bajeti kwa niaba ya wananchi
. Hivyo wengi hawapendi kutokeza katika mikutano ya kimaendeleo “ amesema
mwalingo.
Kwa upande
wa wananchi wameulalamikia uwongozi akiwemo mbunge wa wilaya ya mbeya vijijini
LACSON MWANJALA kwakuwa mbali na wapiga kura wake kwani tangu achaguliwe octoba
30/2010 hajawahi watembelea wala kujua matatizo na kero walizonazo na kushindwa
mtetezi wa shida zao
Mmoja wa
wananchi JOSEPH CHAMBELA alisema wamekuwa na matatizo mengi ikiwa na pamoja na
ukosefu wa huduma bora katika hospitali yao haswa ukitumia huduma ya bima ya
afya na ukihudumiwa utaambiwa hakuna dawa hivi tunatibiwa bule? Alihoji CHEMBELA
Matatizo
mengine ni pamoja na gari la wagonjwa na tunapotaka huduma kwa mama wajawazito
na wakati mwingine kuambiwa halina mafuta pia kutopata pembejeo za kilimo
mbolea kwa wakati na kwa bei kubwa wakati mazao yanapovunwa huuzwa kwa bei ya
chini hivyo kupelekea mkulima kutonufaika na kilimo.
Mwisho
wananchi walishauri wilaya ya mbeya vijijini igawe upya kwakuwa ni kubwa sana
na kupelekea baadhi ya vijiji kushundwa kupata huduma muhimu kwakuwa
zinapatikana mbali, Pia kumpunguzia kajukumu Afisa mtendaji wa kata hiyo
anayetumikia vijiji viwili na anaishi mbali na kata anayofanya kazi.
0 comments:
Post a Comment