SAKATA LA KUGOMA KWA MADAKTARI LIME CHUKUA SURA MPYA MKOANI
MBEYA MARA BAADA YA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KUWAFUKUZA NA KUWARUDISHA
KWA MWAAJIRI WAO KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KWA HATUA ZA
KINIDHAMU NA WALE WAISHIO HOSTELI KUONDOKA MARA MOJA IFIKAPO SAA KUMI NA MOJA NA
KUVIACHA VYUMBA KUWA WAZI.
JANA WALIONEKANA MADAKTARI HAO WAKIHAHA KUTAFUTA HIFADHI YAO
NA MALI ZAO ILI KUTII AMRI ILIYOTOLEWA NA HOSPITALI YA RUFAA ILIYOWATAKA
KUONDOKA MARA MOJA, HALI HIYO IMEJITOKEZA KUTOKANA NA MSUGUANO KATI YA SERIKALI
NA MADAKTARI HAO NCHI NZIMA WAKIDAI BAADHI YA HAKI ZAO.
MADAKTARI WAMEKUWA WAKIENDESHA MIGOMO ILI KUSHUNIKIZA
SERIKALI KUWATIMIZIA MATAKWA YAO HAYO,NA HII NI MARA YA PILI KUFANYA MGOMO WA AINA HIYO
KWANI MNAMO MWEZI MARCH KULIENDESHWA MGOMO KWA MADAKTARI NAKU SABABISHA VIFO NA ADHA KUBWA KWA WANACHI WA TANZANIA.
MNAMO JUNE 23 MWAKA HUU KAMATI YA MADAKTARI ILIBADIKA TANGAZO
LAKUANZA MGOMO USIO NA KIKOMO KITU AMBACHO KILITEKELEZWA KWAKUTOKUINGIA KAZINI
.
HATAHIVYO MNAMO JUNE 28 MWAKA HUU BODI YA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA ILITOA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU YA KAZI JUU YA MGOGORO WAO HUO KWA
KUYABANDIKA IKIWATAKA WASISHIRIKI MAANDAMANO WALA MGOMO WOWOTE NAKISHA KUTOA WARAKA WAKUWAFUKUZA
MADAKTARI HAO.
Hili ni Tangazo liliwataka madaktari kuanza mgomo Hospitari ya Rufaa Mbeya,
PRESS RELEASE
MADAKTARI WA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA
KUTOTEKELEZA WAJIBU WAO WA KUHUDUMIA WAGONJWA.
Tarehe
22/6/2012 mahakama kuu ya kazi Tanzania (The high cout of Tanzania labour
division of the high court at Dar es salam) ilitoa hukumu na. 73 ya 2012(miss
Appl no.73 of 2012 kwenye kesi kati ya
mwanasheria mkuu wa serikali (Attomey general na chama cha madaktari Tanzania
(Medical Association of Tanzania (Mat) hukumu hiyo iliamuliwa wanachama wa MAT nchi
nzima wasifanye wala kushiriki kwenye
mgomo. Ninanukuu (I therefore, based on the afore stated reasons do hereby grant
the application order temporary injunction the following effect;
That the
respondent and its members country, are restrained from colling or
participating the strike pending the determination of the application into
parties it is so orderd S.C Moshi
Judge
22/6/2012
Hukumu hiyo
ilijulishwa kwa wafanya kazi wote hata hivyo,Kuanzia june23mwaka huu Siku ya
jumamaosi asubuhi yalibandikwa matangazo sehemu mbalimbali za Hospitali ya Rufaa
ambayo yaliwaasa wafanyakazi wagome hayakuwa yameonyesha kuwa yametolewa na
nani ila tu ilionyesha imetolewa na KAMATI
Siku hiyo yajune
23mwaka huu Wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctor 12 na Registrars 3)
hawakufika kazini Tarehe 24/6/2012 wafanya kazi 19 Intern Doctors 15 Registrars
4) hawakufika kazini na kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo Imethibitika kuwa
Intern Doctors 54 Registrars 18 hawakufika hadi leo Tarehe 28/6/2012.
Tarehe
25/6/2012 Bodi ya hospital ilifanya kikao cha dharura hali ya utendaji kazi na
utaoji wa huduma hospitalini. Bodi iliamua yafuatayo
1. Mwenyekiti wa bodi akutane na
madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na
kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo.
2. Madaktari wote ambao hawafiki kazini
waandikiwe barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa
kuvunja mkataba walioingia na Hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za
utumishi wa umma Toleo la 2009, kifungu na. f 16-f 17 na f 27
3. Iwapo madaktari ambao hawafiki kazini
hawataripoti au kueleza sababu za kulidhisha ifikapo Tarehe 28/6/2012
kwakuzingatia kanuni za utumishi wa umma toleo la 2009 kifungi na. 16-17 na f
27 madaktari hao watakuwa wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwaajiri wao
ambaye ni Katibu mkuu wa wizara ya Afya ustawi wa jamii kwa hatua zaidi za
kinidhamu zinazostahili
4. Bodi iliwasiliana na Taasisi
mbalimbali hapa Mbeya na nje ya mkoa ili kupata wafanyakazi wa kusaidia
kupunguza makali ya katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Matokeo ya maamuzi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)
Madaktari
wote walioalikwa kukutana na mwenyekiti wa Bodi ya hospitali Rufaa Mbeya hawakuhudhuria
(ii)
Barua
walizo andikiwa ili kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa
kutofika kazini hazikujibiwa.
(iii)
Tumepata
ushirikiano toka kwa mkurugenzi wajiji kwa kupatiwa madaktari watano kusaidi
hospitali ya Rufaa
Leo Tarehe 28/6/2012
madaktari Intern 54 wanapewa barua zao za kuwaeleza kuwa Bodi ya hospitali ya
Rufaa Imesitisha Internship yao hapo hospitalini na kuwarudisha kwa Katibu Mkuu
wa wizara ya Afya na ustawi wa jamii kwa hatua zaidi zinazosthili. Hivyo kwa
wale wanao kaa Hostel waondoke kabla ya saa kumi na moja jioni leo.
Madaktari waajiliwa
wanakabidhiwa Barua zao za kusimamishwa ajira yao katika hospitali ya Rufaa
Mbeya na kurudishwa kwa Katibu mkuu wa
wizara ya Afya na ustawi wa jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu.
Aidha wote wanapaswa kukubidhi mali
zote za Hospitali.
Madaktari wakijiandaa kuondoka katika Hostel ya Hospitali ya Rufaa Mbeya. Wakitii Amli ya kuwataka kufanya hivyo.
MADKTARI WA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WAKIONDOKA ENEO LA HOSTEL MARA BAADA YA KUONDOLEWA NA BODI YA HOSPITALI HIYO
0 comments:
Post a Comment