Amani,
utulivu na Maendeleo ya nchi haviwezi paitikana bila waandishi wa Habari, Hayo
yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa mbeya Diwani Athumani katika kikao cha
pamoja alipowatembelea katika ofisi ya Clubu ya waandishi wa Habsri zilizopo
uhindi jijini mbeya.
Diwani
alifika ofisini hapo kwa malengo ya kujitambulisha kwa waandishi wa habari mara
baada ya kuondoka kwa kamanda Advoket Nyombi na nafasi yake kuchukuliwa naye.
Aliwataka waandishi wa habali kutoa ushilikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha
jiji kuwa katika hari ya usalama na amani.
“Ninajua
waandishi wa habari ni makachelo na mnapata taarifa nyingi kuliko hata jeshi la
Polisi, Tukishilikiana kwa pamoja tutakomesha vitendo vya uharifu vilivyoshamiri
mkoani mbeya, Tukifanya hivyo tutaisaidi jamii kupata haki zao ambazoziko
hatalini kupotea, Kwaupande wa jeshi la polisi tumejipanga sana” amesema
Diwani.
Kwaupande wa
waandishi wa habari wamempongeza kamanda Diwani kwakutambua umuhimu wa Tasinia
hii ya Habari na kwatembelea katika Clubu yao ili kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano kama
alivyotaka lakini walimuomba kutokuwa na ubaguzi kwa kuwataka baadhi ya
waandishi na wengine kuona kama hawafai kwakufanya hivyo kutamfanya afanye kazi
kwa uguma sana.
0 comments:
Post a Comment