Maandishi wa
habari Baraka fm Radio wametakiwa kuyatumia vema mafunzo waliyoyapata katika
semina ya wiki tatu yaliyo tolewa na wawezeshaji toka Farm Radio International
ya jijini Arusha ili kuwajengea uwezo wa kuandaa vipindi vyenye ubora
Akiongea Mgeni
Rasmi wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Radio hiyo
Charles Mwakipesile aliwataka waandishi kuitumia taaluma yao kwakuelimisha
jamii na kuondokana na mambo ya uchochizi kwani kwa kufanya hivyo kalamu yao
inaweza kuliangamiza Taifa.
“Ninawapongeza
kwa kupata mafunzo haya ninaimana kupitia Elimu hiyo mtakuwa na vipindi vizuri
vitakavyo toa elimu na kupendwa na jamii, Lakini pia kupitia semina hii
mkaheshimu taaluma zingine kwakujari misingi na viapo vyao, msiingize ushabiki
katika migogoro ya sekta zingine zitakazo leta uchochezi kwa Taifa” alisma
Mwakipesle
Kwaupande wake
muwezeshaji wa mafunzo hayo Ester Mwangabula aliwasihi waandishi kwakupitia
mafunzo hayo watunze sana vyeti walivyopata kwani vinaweza kuwapa sifa za
kufanya kazi na mashilika mengine mbali na kuajiliwa na kituo cha Radio.
Waandishi wa
habari kumi (10) wamepata mafunzo hayo ya kujengewa uwezo wa kuandaa vipindi
vilivyo bora katika Radio sana vile vya kilimo, wamejifunza jinsi ya kuandaa
vipindi ya kurekodi,kuaandaa script na editing voice
0 comments:
Post a Comment