Katika hali isiokuwa yakawaida
mwanamke mmoja mkazi wa Isanga jijini Mbeya amejitosa kwenye kazi iliyozoweleka
na wanaume yakuendesha bajaji ili kujikwamua kimaisha.
Mwanamke
huyo mkazi wa Isanga Jiji Mbeya Jasmini konga amesema hayo wakati akiwa katika shughuli
zake akizungumza na blog ya malafyale na kuwataka wanawake kuondokana na matazamo
potofu kuwa kuna kazi zinazo fanywa na wanaume tu.
Jasmini
amesema kilichomvutia kufanya kazi ya kuendesha bajaji ni kutaka kuona kwamba
hata wanawake wanaweza na pia ameipenda kwakua inamsaidia kupata kipato sha
kujikimu kimaisha akisaidiana na mume wake kuendesha maisha ya kila siku
nakuongeza kuwa muda mlefu alikuwa akiitamani kazi hiyo hivyo anafurahia kutimiza ndoto yake.
Amesema
licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo akiwa barabarani bado hakati taamaa
ikiwemo kuwahi kupaki mapema bajaji yake kutokana na majukumu mengine ya
kutunza familia kwani ana mume na mtoto hivyo kusababisha wakati mwingine
kutofikisha malengo ya tajiri yake.
Mwanamke huyo amesema malengo yake ya baadae
ni kuona anamiliki Bajaji yake mwenyewe ili kuwa huru zaidi kwa kijiajiri na
kupata kipato chake.
Naye Abdalla
Muhamed mmoja wa madereva hao ameitaka jamii kuheshimu kazi za madereva hao
kwani inawapatia kipato chao cha kila siku hivyo kuizarau ni kuwakatisha tamaa
vijana .
0 comments:
Post a Comment