Pages

Ads 468x60px

Tuesday, October 23, 2012

MTANGAZAJI WA BARAKA FM RADIO AONDOKANA NA USIMBE SHEREHE ZA KUMUAGA ZAFANYIKA KIJIJINI KWAO ILEJE



Mtangazaji  anaye endesha vipindi vya Habari na matikio pamoja na hapa na pale Mpoki Japhet afunga pingu za maisha na kuanza maisha mapya ya kujenga familia yake shehehe za kumuaga zafanyika kijijini kwao ileje mwishoni mwa wiki hii.

Sherehe hizo zilifana sana na kuhudhuruwa na wachungaji wafanyakazi wa Baraka fm radio ndugu jamaa ma marafiki wa karibu ambapo Mpoki amewashukurusa kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha kwake  kwa kufanikisha shughuri hiyo ambayo  ameona kama muujiza.

Kwa upande wa msemaji wa ukoo wa mzee Japhet Kalinga amempongeza binti yao kwakutunza maadili waliyokuwa wakimfundisha na kuwafanyia heshima kubwa ya kumpata mwenzi wake  kwa utaratibu wa mila na desturi za jamii nzima, Ameongeza kuwa imekuwa na jambo la kawaida kwa mabinti wa sikuhizi kujiozesha bila kufuata taratibu.

Nao ndugu jamaa na marafiki waliofika katika sherehe hiyo wamemtakia heri na baraka ya maisha mema katika safari hii mpya na muhimu katika maisha ya mwanadamu katika kujenga familia yake

Mpoki Japhet ambaye amefunga ndoa na Godlove Senyela wa forest jijini mbeya, wakitimiza maandiko ya mungu yanayosema kwahiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja. 



HII NDIYO HARI HALISI YA SAFARI YA KUELEKEA ILEJE KWENYE SHEREHE ZA KUMUAGA MPOKI JAPHET
MPOKI JAPHET AKIWASHUKURU WAGENI WAALIKWA WALIOFIKA KATIKA SHEREHE ZA KUMUAGA KIJIJINI KWAO ILEJE

MUME WA MPOKI JAPHET GODLOVE SENYELA

 MPOKI JAPHET NA MUME WAKE GODLOVE SENYELA WAKIWA NA WAPAMBE WAO

                         MPOKI JAPHET AKIWASILI UKUMBINI ILI KUANZA SHEREHE
MPOKI AKIMTAFUTA MUME MTARAJIWA KATIKATI YA UMATI WA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA TENDO HILO
MPOKI AKIMBUSU MUMEWE MTARAJIWA MARA BAADA YA KUMPATA KATIKA UMATI MKUBWA WA WATU
MTOTO WA KINDALI AKIMKABIDHI ZAWADI YA BUYU LILILOJAA MAZIWA YA MGANDO MUME MTARAJIWA

              BAADA YA KUNYWA DU! MATAM ASANTEEE NI MANENO YA GODLOVE


MBWEMBWE ZA MC OBADIA HAZIKUWA NYUMA KATIKA KUSHEREHESHA SEND OF HIYO KATIKA KUFUNGUA SHAMPENI



ILIFIKA WAKATI WA KULISAKATA LUMBA LILIFUGULIWA NA MAARUSI WENYEWE HARI ILIKUWA KAMAUNAVYO TAZAMA HAPA

0 comments:

Post a Comment