Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Philipo Mulugo akizungumza na waandishi wa habari |
Mtihani
wa
Kidato cha Nne mwaka 2012 utafanyika nchini kote kuanzia tarehe 08,
hadi
tarehe 25 Oktoba, 2012. Jumla ya watahiniwa walioandikishwa kufanya
mtihani ni 481,414 wakiwemo wavulana 263,202 sawa na asilimia 54.67 na
wasichana 218,212 sawa na asilimia 45.33.
Idadi hiyo ya watahiniwa wote walioandikishwa mwaka 2012 ni ongezeko la
watahiniwa
31,090 sawa na asilimia 6.90 ikilinganishwa na watahiniwa 450,324
walioandikishwa kufanya mtihani
huo mwaka 2011. Watahiniwa wote
walioandikishwa kufanya mtihani mwaka 2012 wamegawanyika katika makundi
matatu
kama ifuatavyo:-
·
Watahiniwa
wa shule (School Candidates)
ni 412,594 wakiwemo wavulana 228,991 sawa na asilimia 55.50 na wasichana
183,603 sawa na asilimia 44.50. Watahiniwa hao wa shule wa mwaka 2012
ni
ongezeko la watahiniwa 63,204 sawa
na asilimia 18.09 ikilinganishwa na
watahiniwa wa shule 349,390 wa mwaka 2011.
·
Watahiniwa
wa Kujitegemea (Private Candidates)
ni 68,820 wakiwemo wanaume 34,211 sawa na asilimia 49.71 na wanawake
34,609 sawa na asilimia 50.29.
Watahiniwa wa Kujitegenea walioandikishwa mwaka 2012 ni pungufu ya
Watahiniwa 32,114 sawa na upungufu wa asilimia 31.82 ikilinganishwa na
watahiniwa 100,934 walioondikishwa mwaka 2011.
·
Mtihani wa
Maarifa (Qualifying Test) utafanyika
tarehe 16 Oktoba, 2012. Jumla ya watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa
walioandikishwa ni 21,314 wakiwemo wanaume
8,174 sawa na asilimia 38.35 na wanawake 13,140 sawa na asilimia 61.65.
Watahiniwa wa Maarifa walioandikishwa mwaka 2012 ni pungufu ya
watahiniwa 8,133 sawa na upungufu wa asilimia 27.62 ikilinganishwa na
watahiniwa 29,447 walioandikishwa mwaka 2011.
Watahiniwa
wote wameandikishwa katika shule/vituo vilivyotawanyika katika Mikoa mbalimbali
nchini kama ifuatavyo:- Jumla ya shule 4,155 zina Watahiniwa wa Shule (School
Candidates). Watahiniwa wa Kujitegemea (Private candidates)
wameandikishwa katika vituo 902; na Watahiniwa
wa Maarifa (Qualifying Test) wameandikishwa katika vituo 616.
Ndugu
wananchi,
Hadi
sasa maandalizi na usafirishaji wa mitihani hiyo hadi ngazi ya mikoa yamekamilika.
Aidha, mikoa inaendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa kila kituo kinapata
mitihani yake kwa muda uliopangwa kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya
Baraza la Mitihani la Tanzania.
Ndugu
Wananchi,
Kuhusu
usalama wa mitihani, hadi sasa mitihani yote ipo salama, na hakuna mtihani
uliyovuja katika ngazi yoyote kuanzia Baraza la Mitihani, Mikoa na Halmashauri.
Ninatoa pongezi kwa Baraza la Mitihani kwa kuandaa mitihani hiyo na
kuisafirisha kwa usalama hadi ngazi ya mkoa.
Ninatoa
wito kwa Kamati za Mitihani za mikoa yote kuhakikisha kuwa taratibu zote za
utunzaji, uhifadhi na usafirishaji wa mitihani hiyo zinazingatiwa. Ni matumaini
yangu kuwa ufuatiliaji na ukaguzi wa usalama wa kila kituo umefanyika na hatua
za kurekebisha mapungufu kama yapo zimefanyika.
Ndugu
Wananchi,
Mtihani
wa Kidato cha Nne ni muhimu sana kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwani
hutumika katika uchaguzi wa watahiniwa wanajiounga na masomo ya Kidato cha Tano
na Vyuo mbalimbali. Aidha, ili kuweza
kujiunga na soko la ajira katika taasisi za umma au sekta binafsi ni lazima
mhusika awe na cheti cha Kidato cha Nne.
Hivyo mtihani wa Kidato cha Nne ni muhimu sana kwa maisha ya watahiniwa
na wananchi kwa ujumla.
Ndugu wananchi
Ufanisi
wa zoezi muhimu kama la mitihani unahitaji ushirikiano wa wadau wote. Ninatoa
wito kwa wananchi wote, wakiwemo Viongozi, walimu, Wazazi, Jamii na Wasimamizi wa mitihani kutoa ushirikiano wa
kutosha na kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa ya amani na utulivu kipindi
chote cha mitihani. Wakuu wote wa vituo vya mitihani hakikisheni kuwa mahitaji
yote ya msingi kuhusu mitihani yanapatikana.
Ndugu
Wananchi,
Kutokana
na muhimu wa mtihani wa Kidato cha Nne katika
kutoa mwelekeo wa maisha ya
watahiniwa kama ilivyofafanuliwa hapo juu, wapo baadhi ya watahiniwa na
wasimamizi wasio waaminifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya
udanganyifu katika mitihani. Watahiniwa
wanaobainika kufanya udanganyifu katika mitihani wamekuwa wakifutiwa matokeo
yao yote ya mitihani kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji wa Mitihani ya Taifa.
Ninachukua
fursa hii kuwakumbusha watahiniwa kuwa, kila mtahiniwa afanye mitihani yake kwa
kujitegemea bila udanganyifu. Wale wote watakaobainika kushiriki katika udanganyifu
watachukuliwa hatua za kinidhamu. Nikirejea mtihani wa mwaka 2011, jumla ya
watahiniwa wa Kidato cha Nne 3,303
walifutiwa matokeo yao kwa sababu ya kufanya udanganyifu. Aidha, walimu waliohusika
walipewa adhabu mbalimbali ikiwemo onyo, karipio kali, kuvuliwa madaraka wakuu
wa shule na wengine kushitakiwa TSD. Aidha, wenye shule waliothibitika
kusababisha udanganyifu wameandikiwa barua ya kusudio la kuzuia kudahili
wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa muda wa mwaka mmoja.
Kuhusu
watahiniwa waliofutiwa matokeo, baada ya kuomba msamaha wamepunguziwa adhabu,
na wataruhusiwa kufanya mtihani mwaka 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea baada
ya kutumikia adhabu kwa muda wa miaka miwili. Ninatoa wito kwa walimu, viongozi
na wazazi kuwaasa watahiniwa kuhusu swala la udanganyifu, kwani kwa mwaka huu
adhabu haitapunguzwa. Ni matumaini yangu kuwa watahiniwa wote watazingatia taratibu
zote za mitihani bila kujiingiza katika udanganyifu. Serikali haitasita
kuchukua hatua kama ilivyokuwa mwaka 2012.
Ndugu
Wananchi,
Ninarudia
kutoa wito kuwa walimu, wasimamizi wa mtihani, Wakuu wa Shule, viongozi wote,
na jamii kutoa ushirikiano na kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika katika
mazingira yenye usalama na amani. Ninaomba
wote tuungane kuwaombea Watahiniwa wetu Baraka za Mwenyezi Mungu na mafanikio
katika mitihani yao.
Ndugu Wananchi,
Katika
kuhitimisha taarifa yangu ninapenda pia kutoa ufafanuzi kuhusu Mtihani wa Taifa
wa Kidato cha sita kwa wanafunzi walioko kidato hicho mwaka 2012/2013.
Wanafunzi hao watafanya Mtihani wa Taifa mwezi Machi, 2013. Aidha, wanafunzi
waliopo kidato cha 3 mwaka huu watafanya Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4 mwezi
Novemba 2013 kama ilivyoelekezwa na Kamishna wa Elimu kwenye Waraka wa Elimu
Na. 5 wa Mwaka 2012 kuhusu Marekebisho ya Mihula ya Shule za Sekondari na Vyuo
vya Ualimu.
PHILIPO A. MULUGO (Mb.)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
0 comments:
Post a Comment