Baadhi ya vijana wanao chimba kokoto maeneo ya Uyole jijini mbeya kwa kutumia zana zisozo rasmi kwa kazi hiyo wapo hatarini kuhatalisha maisha yao ya kuangukiwa na vifusi vya mawe.
Kwamjibu wa
uchunguzi ulio fanywa na mwandishi wa blog hii umebaini kuwa, wachimbaji hao
wanatumia njia ya kuchoma moto mataili ya magari kwa ajili ya kuyalainisha mawe
hayo ili kuwarahisishia kupasua.
Wasiwasi
mkubwa unakuja pale ambapo vijana hao wanaingia chini ya shimo la kuchimba
kokoto huku ukuta ukiwa na ufa mkubwa ambao muda wote unaweza kupolomoka na
kuhatalisha kifo.
HII NDIYO HALI HARISI YA UCHIMBAJI WA KOKOTO MAARUFU KAMA SHIMONI HUKO UYOLE JIJINI MBEYA
HATARI YA MACHIMBO HAYO YANAYOZALISHA KOKOTO ZINAZOTUMIKA KATIKA KUJENGA MAJENGO YA JIJI LA MBEYA
BAADA YA KUZALISHWA TAYALI KWA MATUMIZI YA UJENZI
Nitumaini langu machimbo hayo yanajulikana na maraka husika lakini yatachukuliwa hatua sitahiki mala baada ya kutokea maafa kwakua ndiyo destuli ya waliopewa dhamana wa nchi hii
0 comments:
Post a Comment