Pages

Ads 468x60px

Tuesday, February 26, 2013

AJALI YAMPOTEZA MWANASHERIA WA MANISPAA YA MTWARA




Ajali mbaya imetokea jana jioni mtwara maeneo ya msijute ikiwaua Mwanasheria wa Manispaa-Bw Joachim Lewanga Shayo aliyekuwa akielekea Masasi na Dereva bajaji wake na kumvunja viungo mwanamke mmoja baada ya kugongana uso kwa uso na  gari la pili  la tanesco makao makuu likija mtwara. Ajali imetokea maeneo ya Hiyari/Msijute wakati Marehemu alipokuwa akitaka kulipita gari lingine ndipo wakakutana uso kwa uso. Taratibu za msiba zinaendelea nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mangowela-Mtwara. Kwa walio Mtwara na kwingineko tafadhali mjulishe ndugu jamaa na marafiki na wenye kuitakia mema familia ya Marehemu Shayo.
BWANA ALITOA BWANA AMETWA JINA LA BWANA LIBALIKIWE

0 comments:

Post a Comment