MCHANGO HUO UMEFANYIKA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA
KATIKA VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE JIJINI HAPA NA KUPATIKA ZAIDI YA SHILINGI
MILIONI TATU
Akiongea na wananchi
waliofulika kusikiliza hotuba hiyo iliyotolewa na mwaenyeti wa chama hicho
PHILIMON MBOWE amewatake wananchi kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo
yenye lengo la kushinikiza waziri wa Elimu SHUKURU KAWAMBWA pamoja na naibu
wake
PHILIP MURUGO kujiuzuru kutokana na matokeo
mabovu ya wanafunzi wa kidato cha nne
Mbowe amewataka wabunge waote
kuratibu maandamano hayo na wanafunzi waliofeli kidato cha nne, waalimu, na
wanavyuo kujitokeza kwa wingi barabarani kuunga mkono mpango huo
“Kazi ya kwanza ninayo wapa
nyie wabunge wote mliopo hapa ni kuratibu maandamano hayo ambayo tumeipa siku
kumi na nne Serikali kuwawajibisha mawaziri wa wizara ya Elimu na mafunzo ya
ufundi bado siku tatu kutimia” MBOWE alisema
Ninachosema si utani Mungu
anataka kufanya mabadiliko katika nchi hii anakitumia chama cha chadema kufikia
lengo la Mungu hivyo hatuko tayali
kufanya mzaha katika jambo hili lazima watu hawa wawajibike ama Serikali
iwawajibishe kwakuwa wameshindwa kufanya
kazi wameidhalilisha elimu ya Tanzania
Akitoa takwimu ya ufaulu wa
wananfunzi wa darasa la saba MBOWE amesema kila mwaka wanafunzi mlioni moja na
laki mbili hufanya mtihani wa kumaliza Elimu hiyo ni lakitano tu wanaofauru
kwenda kidato cha nne na laki saba hubaki n a hawa na watoto wa mlala haoi
Kwa wale wanaopata nafasi ya
kufauru kwenda kidao cha nne hupelekwa katika shule za kata kusiko kuwa na
madarasa, vitabu, wala maabara za kujifunzia hali hii tutakuwa nayo mpaka lini?
MBOWE alihoji
0 comments:
Post a Comment