SHINDANO HILO
NI KWA HISANI YA CHAMPION PROJECT
Engender Health kwa
kushirikiana na shirika la FHI 360 ndilo shirika lenye mradi huu wenye kulenga
kuwashirikisha wanaume katika namna iliyochanya kwenye mapambano dhidi ya
maabukuzi ya VVU nchini Tanzania
Mrad huu upo katika mikoa
kumi yenyemaambukizi ya juu ya VVU kwa malengo ya kuhamasisha wanaume kupunguza
uwezekano wa kuwa na wapenzi wengi
Kwa imani kwamba endepo
mwanaume akijua umuhi wa kupunguza kuwa na mahusiano na wapenzi wengi kunaweza
kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha maambukizi ya VVU hapa nchini
Majukumu ya shirika hili ni
kupambana na Mira na desturi zenye kupelekea kuhatalisha maambukizi ya VVU,
Kuhamasisha wanaume kuhudhuria katika huduma za Afya ya uzazi na mototo wakiwa
na wenzi wao, Kuweka sera mahara pa kazi kuhusu wanaume na maambukizi ya VVU
nk,
Katika semina hiyo iliyo
fanyika katika ukumbi wa IFISI COMMUNITY CENTER uliopo Mbalizi Mbeya vijijini
imeendeshwa na muwezeshaji kutoka shirika hilo
MUGANYIZI MUTTA na kuhudhuriwa na waandishi wa habari mkoani hapa amewataka
waandishi wa vyombo mbalimbali, kuandaa vipindi vyenye kuhamasisha wanaume
kuhudhuria katika vituo vya Afya ya uzazi wakiwa na wenzi wao.
Muganyizi ameongeza kuwa
endapo mwandishi ataandaa kipindi cha aina hiyo na kurushwa katika chombo chake,
kipindi hicho kitaingizwa katika shindano hilo na mshindi wa kwanza
atajinyakulia kiasi cha shilingi laki nane, wapili washindi wawili kila mmoja
shilingi laki nne na elfu theanini na wa washindi tatu watapata kiasi cha
shilingi laki tatu na elfu ishilini kila mmoja wapatao wawili.
Shindano hilo litaanza mnamo
April 01-Aprili 30/2013
MWANDISHI WA HABARI WA BOMBA FM RADIO EZEKIELI KAMANGA AKICHORA MFANO WA MTU ILIKUFIKISHA UWA SOMO HUSIKA
WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO VYA HABARI MBALIMBALI MKOANI MBEYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI SEMINA HIYO
WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHURIA SEMINA HIYO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA MAPUMZIKO
BAADA YA KUMALIZA SEMINA WAANDISHI WA HABARI HAWAKUACHA KUONYESHA UMAHILI WAO KATIKA VITUKO
IFISI COMMUNITY CENTER WALIPOFANYIA WAANDISHI WA HABARI SEMINA HIYO
0 comments:
Post a Comment