Akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake mratibu wa huduma hiyo PRISCA BUTUYUYU amesema kumekua na
upungufu mkubwa kwa baadhi ya wanaume kutoshiriki katika huduma za afya ya
uzazi.
“Katika tafiti zilizofanywa
kwa wilaya nane za mkoa wa mbeya tangu mwaka 2009 hadi 2011 zimeonyesha idadi za wanawake wanaokwenda
klinic wakiwa na wenzi wao imendelea kuporomoka kila wakati hivyo ofisi yetu
imeliona hilo na umuhimu wake hivyo kuchukua jukumu la kuhamasisha wanaume kushiriki
katika hupata huduma za afya wakiwa na wenzi wao” BUTUYUYU amesema.
Kunafaida kubwa kwa wenzi
kushiriki pamoja katika huduma za afya
ya uzazi kama vile kupima pamoja,
hususani maambukizi ya VVU kwani kwa kufanya hivyo mnaweza kujitambua na kuishi
maisha ya kumlinda mtoto pamoja na mwenzi wake endapo mmoja wao atagundulika
ana maambukizi, BUTUYUYU amesea
Ameongeza kua mbali na kupima
magonjwa pia kunaelimu mbalimbali ikiwemo kujifunza namana ya kupanga uzazi,
jinsi ya kulea mimba kujiandaa kupokea
mtoto atakapozaliwa pamoja na jinsi ya
kumlea.
Kwakuona umuhimu wa swala
hilo kwa wananchi wa TANZANIA , ENGENDER HEALTH kwa kushirikiana na shirika
la FHI 360 limetoa mradi wa champion wa kuhamasisha
vyombo mbalimbali vya habari kushiriki katika kampeni hii ili kuandika habari pamoja na vipindi vyenye kutoa ujumbe
wenye kuhamasisha wenza kushiriki katika huduma za afya ya uzazi,
Akiongea katika semina ya
waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa IFISI COMMUNITY CENTER
afisa mratibu mwandamizi wa mradi wa champion MUGANYIZI MUTTA amewataka
waandishi kushiriki katika kampeni hizi.
“Mradi huu upo katika mikoa
kumi yenye maambukizi ya juu ya VVu, kwa hiyo tumelenga katika kuhamasisha wanaume
kupunguza kuwa na mahusiano ya wanawake wengi, kupambana na mila na desturi
katika jamii, Kuweka sera mahari pa kazi kuhusu swala la wanaume na maambukizi
ya VVU” amesema MUGANYIZI.
Ameongeza kuwa habari zilenge
kuhamasisha mambo hayo muhimu na mwandishi
atakaye andika habari na ikatumika
katika chombo chake itakuwa imeinga katika shindano la Champion ambalo zaidi ya
Tshs milioni mbili kushindaniwa.
0 comments:
Post a Comment