Edward Moringe Sokoine (1938 - 12 Aprili 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.
Aliwahi
kuwa Waziri
Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari
1977 hadi 7 Novemba 1980, tena tangu tarehe
24
Februari 1983
hadi kifo chake,
alipofariki kufuatana na ajali ya gari. Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi
alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi
huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma. Sokoine alifariki
kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es
Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa. Kifo chake kilileta
majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea
wanyonge na kuinua hali ya maisha yao. Mwili wa Edward
Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha.
Chuo cha Kilimo
na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine"
ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
0 comments:
Post a Comment