Pages

Ads 468x60px

Monday, May 20, 2013

Udini ni athari kwa vijana


VIJANA  wa chama cha Mapinduzi  (CCM)  wameaswa kuacha kushabikia udini badara yake  wajadili mambo ya maendealeo na elimu kwa mustakabari wa maisha yao kwani Tanzania ikiingia katika migogoro watakao athirika ni wao.




HUSENI BASHE AKIWASILI NA KUPOKELEWA NA VIONGOZI WA VIJANA KATIKA OFISI ZA CCM MKOA WA MBEYA

BASHE AKISAIN  KITABU CHA WAGENI KATIKA OFISI VIJANA MKOA WA MBEYA



MGENI RASMI HUSEN BASHE AKIPOKELEWA KWA SHANGWE NI VIJANA WA CCM WALIOKUWA WAKIMSUBIRIA KWA HAMU KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO

KIONGOZI WA VIJANA AKIMKABITHI RISALA MGENI RASMI MARA BAADA YA KUISOMA
MWENYEKITI WA VIJANA WA CCM WILAYA YA MBEYA MJINI MATUKUTA MATUKUTA AKITETA JAMBO NA MGENI RASMI KABLA YA KUMKARIBISHA KUONGEA NA VIJANA
MATUKUTA AKIMKARIBISHA MWANYEKITI WA CCM WILAYA  MWAITENDA AMKARIBISHE MGENI RASMI ATOE HOTUBA YAKE KWA VIJANA
MWANYEKITI WA CCM WILAYA YA MBEYA MJINI MWAITENDA AKIONGEA JAMBO KABLA YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI 


HUSEN BASHE AKIHUTUBIA VIJANA WALIOFULIKA KUMSIKILIZA KATIKA UZINDUZI WA BARAZA LA VIJANA


VIONGOZI MBALIMBALI WAKISEMA MAMBO KTIKA UZINDUZI HUO KUPUNGEZA JUHUDI ZA VIJANA




Udini ni athari kwa vijana
VIJANA  wa chama cha Mapinduzi  (CCM)  wameaswa kuacha kushabikia udini badara yake  wajadili mambo ya maendealeo na elimu kwa mustakabari wa maisha yao kwani Tanzania ikiingia katika migogoro watakao athirika ni wao.

Hayo yamesemwa na Mjumbe mkuu wa CCM taifa Bw. HUSEN BASHE akiwa mgeni rasmi Kwenye Uzinduzi wa  baraza la vijana wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya mbeya mjini mwisho ni mwa wiki katika ukumbi ccm mkoa.

Bashe amewataka vijana kuachana na kushabikia migogoro ya kidini iliyoibuka hivi karibuni  katika taifa la Tanzania. Akilinganisha na nchi jirani ya Kenya wao wanajadili kuboresha elimu yao watanzania wanashindana nani achinje.

“Nataka kuwaambia vijana wenzangu watakao leta mabadiliko katika nchii ni sisi vijana tuliopo sasa tuachane na ushabiki utakaotuharibia maisha ya miaka hamsini ijayo ambayo ndiyo tutakayo ishi sisi tutakuja kulaumiwa na kizazi kijacho kama hatutailinda amani hii waliyotutengenezea wazee wetu walipita” Bashe amesema

Aliongeza kua ajua jimbo hili la mbeya mjini linashikiliwa na upinzani lakini mnakila sababu ya kulirudiaha uchaguzi ujao kwani watanzania bado wana imani na chama cha mapinduzi na kitaendelea kutawala miaka hamsini mingine ijayo.

Kwa upande wa mchakato wa katiba amewataka vija kujiaandaa kiseikolojia kukabiliana na babadiliko yoyote yatayo jitokeza na kua makini kwani yawezekana kukatokea kuvunjika kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar au kukawa na  serikali tatu jambo la kujiuliza je Tanzania inauwezo wa kuendesha serikali tatu? Mwaisho Bashe aliwachangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajiri ya baraza hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya mbeya mjiniMatukuta Matuku  alimpongeza sana mgeni rasmi huyo kwa moyo wake wa dhati kwa kuwapenda vijana na kuwa tayali kuwa sidia katika baraza lao japo kua iliku gafra lakini akakubari kulifungu baraza lao hilo

0 comments:

Post a Comment