Mwili wa Pepetua Maina ukiwa katika shimo la taka.
|
MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy,
Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa
amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka.
Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa
msichana huyo ulionekana na mfanyakazi mmoja wa ndani wakati akienda
kutupa takataka eneo hilo ambapo alipouona alipiga kelele zilizowafanya
majirani kukimbilia eneo la tukio na kujionea wenyewe.
Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.
Mwili
wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu Mikocheni B, jirani
kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova.
...Mwili wa Pepetua baada ya kufunikwa.
Taarifa
za kipolisi zilidai kuwa mrembo huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa kwani
mkono mmoja wa kushoto ulivunjika na kukutwa na jeraha kubwa katika
paji la uso.Wakizungumza na Uwazi kwa tahadhari kubwa kuogopa ushahidi, baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema hawakusikia vurugu zozote usiku kwa hiyo huenda wauaji walimchinja mbali na kwenda kuutupa mwili wake eneo hilo.
Mwili wa Pepetua ukitolewa shimoni na polisi.
Juni
9, mwaka huu, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura kuhusu kifo cha msichana
huyo ambapo alikiri kutokea.Kamanda Wambura alisema kuwa, Pepetua alikuwa akifanya kazi kwa Jaji Engera Kileo kwa miaka mitatu mpaka siku ya kifo chake.
Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
“Jeshi
la polisi tulipokea habari za kuwepo kwa mwili huo jana (Jumamosi) saa
sita na nusu, tukaenda na kuukuta ukiwa kwenye shimo la taka
umechinjwa shingoni na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye
ncha kali na kwenye paji la uso alipasuliwa.
...Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.
“Tuliuchukua
na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Mwananyamala. Vijana wawili
wanaoishi kwa Jaji Kileo ndiyo waliofika hospitali na kumtambua
marehemu. Jaji mwenyewe alikuwa safarini nje ya nchi, amerejea leo (juzi
Jumapili).“Mpaka sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho, siwezi kuzungumza kwa undani zaidi,” alisema Afande Wambura.
0 comments:
Post a Comment