Jopo
la Madaktari wakihaha kumpatia huduma ya kwanza, mkimbiaji mwanadada wa
nchini Kenya, Irine Cheptai, aliyeanguka na kuzimia wakati akimalizia
mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki.
Cheptai
akiwa amewekeaa mtungi wa hewa ya oksijeni, baada ya kuanguka na
kuzimia kutokana na shambulio la moyo. Hata hivyo aliweza kupata fahamu
na kuzinduka baada ya kufikishwa hospitali.
Cheptai (wa pili kulia) akikimbia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London.
*********************************
LONDON, England
Cheptai,
binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora
zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini
akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa
kumalizia
MKIMBIAJI
wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya, Irine Chebet Cheptai jana
alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na mshituko wa moyo
kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita 3,000.
Cheptai,
binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora
zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini
akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa
kumalizia.
Madaktari
waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha kumtundikia mtungi wa Oksijeni,
ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo zilipasha kuwa
alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.
Tukio
lake limeshtua wengi kutokana na kukimbia katika mbio fupi kulinganisha
na zile alizozoea za mita 5,000, ambazo ameshiriki Diamond League mara
mbili msimu huu, na anakumbukwa kwa rekodi yake ya dakika 14:50.99
jijini Shanghai, Mei mwaka huu.
Daily Ma
0 comments:
Post a Comment