MFANYA BIASHARA
MAARUFU WA SPEA ZA MAGARI JIJINI MBEYA APIGWA KUTESWA KUVUNJWA MKONO NA ASKARI POLISI KISA ELFU
ISHIRINI TU,
HUKU AKIWA
AMEFUNGWA PINGU ALAZWA KATIKA HASPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI
MFANYA BIASHARA EDWARD MWAISANGO AKIWA CHINI YA ULINZI HUKU AMEFUNGWA PINGU MIKONO YAKE KAMA JAMBAZI SUGU KATIKA KITUO CHA MWANJELWA
ASKALI MESHAKA ANAETUHUMIWA KUMSURUBU VIBAYA MFANYABIASHARA WA SPEA ZA MAGARI EDWARD MWAISANGO AKIANDIAKA MAELEZO KATIKA KITUO CHA MWANJELWA
HII NDIYO GARI YA ASKALI MESHAKI ILIYOTUMIKA KUMCHUKUA EDWARD NA KUANZA KUMWAGIA KIPIGO NDANIA GARI HILI ILIYOPELEKEA MAJERAHA KICHWANI MWAKE.
EDWARD MWAISANGO AMELEZWA KATIKA HAOSPITALI YA RUFAA MBEYA AKIUGULIA MAJERAHA YALIYOSABABISHWA NA KIPIGO CHA POLISI
EDWARD MWAISANGO AKIWA KATIKA MOJA YA VYUMA VYA WAGOJWA KWA AJILI YA MATIBABU
KAKA YAKE JOSEPH MWAISANGO MWANDISHI WA BLOG YA MBEYA YETU AKIONGE KWA UCHUNGU KITU ALICHOTENDEWA MDOGO WAKE KUWA NIKIBAYA NA NI CHA UONEVU
WANAFAMILIA WA EDWARD, JOSEPH MWAISANGO KUSHOTO NA PENIEL MWAISANGO WAKIJADILI JAMBO JUU YA KUPIGWA KWA KWA NDUGU YAO
HABARI ZAIDI
KAURI YA
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YAZIDI KUTEKELEZWA NA JESHI LA POLISI KWA KUWAPIGA
RAIA NCHINI
MFANYA BIASHARA
MAARUFU WA SPEA ZA MAGARI JIJINI MBEYA APIGWA KUTESWA KUVUNJWA MKONO NA ASKARI POLISI KISA ELFU
ISHIRINI
HUKU AKIWA
AMEFUNGWA PINGU ALAZWA KATIKA HASPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI
Mfanya biashara
wa duka la spea za magari Soweto jijini Mbeya Edwardi Mwaisango mwenye umri wa
miaka 40 amelazwa katika Hospitali ya Rufaa mbeya baada ya kukamatwa kuteswa akiwa
kafungwa pingu kuvunjwa mkono na Askari
polisi aliyejulikana kwa jina moja la Meshaki wa kituo cha kati.
Akiongea kwa
maumivu makali hospitalini hapo alipolazwa kisa kilicho pelekea kufanyiwa
vitendo hivyo vya ukatili Edward amesema kua asikali huyo alifika dukani kwake
kwa lengo la kununua limu la gari yake aina ya opa walilokubaliana kwa malipo
ya shilingi elfu thamanini askali huyo alinunua na kuondoka nalo
Baada ya
masaa kadhaa alililudisha baada ya kupata limu lingine lakini hakupewa pesa
zote kwakua zilikwisha tumika kiasi cha shilingi elfu ishili zikasalia na hizo
ndizo zilizopelekea unyama huo.
Edward
aliongeza kua siku ya tukio hilo alichelewa kufika Dukani kwake hivyo alipofika
gafra akatokea askari huyo akiwa na rafiki yake ambae hakujulikana mapema jina
lake ambae alikua ndani ya gari lao aina ya opa
wakamkamata na kumfunga pingu mikono
yake kisha kumpeleka katika kituo kidogo cha mwanjelwa ambako ndiko alikoanza
kupigwa na vitu nigumu vilivyopelekea majeraha mbalimabli katika mwali wake na
kumvunja mkono wake wa kulia
Kamanda wa
polisi mkoa wa mbeya Diwani Athumani amekiri kupokea tukio hilo, na kudai kuwa
kitendo hicho ni kibaya na kudai kuwa suala hilo linafanyiwa uchunguzi na endapo
askari huyo akibainika namakosa atawajibishwa kwa mjibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment