Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 22, 2013

AL SHABAAB WATHIBITISHA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA KIGAIDI NAIROBI.

Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
 
-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia
-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa
KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.

Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shambulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.



Na Kenneth Kinonko  wa Globu ya Jamii, Nairobi
Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa. 
Kupitia ujumbe wao katika mtandao wa twitter, kundi hilo limesema shambulio hilo ni ujumbe kwa Serikali ya Kenya kuitaka iondoe majeshi yake yote kutoka Somalia. Kundi hilo pia limedai kuwa limeua watu zaidi ya idadi inayotajwa na vyombo vya usalama vya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema serikali bado haijabaini ni nani wamehusika na shambulio hilo. 
Wakati huo huo idadi ya watu wanaosadikiwa kuuwawa imetajwa kuwa ni 30 na zaidi ya 50 wamejeruhiwa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa
Wateja wakihaha ndani ya duka hilo
Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba
Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha amedhakufa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu.

Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.

Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake. Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

0 comments:

Post a Comment