Pages

Ads 468x60px

Saturday, October 5, 2013

BASI LA KAMPUNI YA JM LUXURY COACH LILILOPATA AJALI ABIRIA 15 WAJERUHIWA VIBAYA


Wananchi  na kijiji  cha Mazombe  Kilolo  pamoja na abiria  wa basi la JM Luxury Coach  wakilitazama basi  hilo baada  ya  kupinduka  eneo la Mazombe  leo majira ya  saa 11 jioni wakati  likitokea  Dar  kuja  Iringa mjini basi  hilo lenye namba za usajili T 957 CGK
Basi la JM baada  ya  kupinduka
Mmoja kati ya majeruhi  wa ajali hiyo akitoka katika basi la JM baada ya ajali
Majeruhi  wa ajali ya JM akitafuta  mizigo  yake
Abiria  wakitoka katika  basi hilo baada ya kupinduka
ABIRIA  15   waliokuwa  wakisafiri  na basalaam kuelekea  mjini Iringa  wamejeruhiwa  vibaya huku  wengine  zaidi  ya 40  wakinusurika  kifo  baada  ya basi  hilo lenye namba za usajili TT 957 CGK kuacha  njia na kupinduka

Ajali  hiyo  imetokea leo majira ya saa 11  jioni katika eneo la Mazombe Ilula  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  katika barabara kuu ya Dar es Salaam  - Iringa

Mashuhuda  waliozungumza na mtandao huu  wa www.matukiodaima.com eneo la  tukio  walidai kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva  kushindwa  kulimudu gari  hilo.

Kwani walisema  kuwa  eneo hilo lenye  kona dereva  alikuwa katika mwendo na  kuhama njia kabla ya kupinduka na kuwa katika ajali  hiyo watu  15 wamejeruhiwa vibaya na wengine  kunusurika na kuwa majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Jeshi la polisi mkoa  wa Iringa  limethibitisha tukio  hilo na kuwa hakuna aliyepoteza maisha katika ajali  hiyo

BREAKING NEWS ......AJALI NYINGINE TENA USIKU HUU MLIMA WA KITONGA ,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

Haya  ndio magari  matatu  yaliyogongana mlima  Kitonga na  kusababisha  vifo  vya  watu  wawili na  kujeruhi  wawili
Abiria  waliokuwa  wakisafiri  kutoka  Dar na mikoa ya nyanda  za juu kusini wakishuhudia ajali  baada ya  kukwama  eneo la Kitonga  kufuatia ajali  hiyo kuziba njia
Dereva  wa lori IT lililosababisha ajali akiwa amebanwa kwa zaidi ya saa moja katika gari lake
Hivi ndivyo  dereva  huyo aliyefahamika kwa jina la Gody akiwa amebanwa
Gari ndogo iliyonusurika  kugongwa  ikininia katika mlima  Kitonga
Fuso  ambayo dereva na utingo  wake  walipoteza maisha  kwa ajali hiyo
Maiti ya  utingo  wa  fuso iliyogongana uso kwa uso na Lori baada ya  kutolewa katika fuso hilo
Dereva  wa Lori IT ambae  alibanwa na  kuvunjika mguu  wake mmoja papo hapo akitoa maagizo kwa rafiki yake baada ya  kukata  tamaa kama atatoka eneo hilo
Gari  la  polisi  lenye  miili ya marehemu
Abiria  wakitazama ajali  hiyo
Mwili  wa  dereva  wa fuso ukiwa bado kutolewa katika gari baada ya  kubanwa
Dereva  huyo baada ya  kutolewa katika  lori  hilo
Majeruhi  wa ajali hiyo Bw  Gody kushoto akiwa amelala katika gari la polisi pamoja na maiti ya utingo wa fuso
Dereva  Taxi mjini  Iringa Bw  Brawn akilitazama gari la Zimamoto mji Iringa  lililofika  kusaidi kuokoa eneo hilo
Ulinzi mkali ukiwa  umeweka eneo la ajali hiyo
Dereva wa Lori akisaidia  huku mguu mmoja ukiwa umevunjika vipande  vinne
Ajali mbaya  nyingine  imetokea  usiku  huu katika mlima kwa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara  kuu ya Dar es Salaam -Iringa .

Katika  ajali  hiyo  watu  wawili wamekufa papo hapo huku wa wawili  wakijeruhiwa  vibaya baada ya malori mawili kugongana  uso kwa uso .

Ajali  hiyo imetokea  mida ya saa 12.50 jioni ya  leo  ikiwa ni dakika takribani 30  baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo  la Mazome  wilaya ya Kilolo.

waliopoteza maisha katika ajali  hiyo ambayo chanzo ni dereva  wa lori la IT lililokuwa  likisafirishwa kwenda nchi  za  kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka  kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali .

Hata  hivyo  dereva  wa  lori  hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody  amevunjika mguu  wake ambao umetoka katika na  dereva  na utingo la fuso wamekupa papo hapo  huku mwanamke  aliyekuwa katika lori IT akisalimika .

habari zaidi itakujia

0 comments:

Post a Comment