Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 16, 2013

HII NDIO SABABU ILIYOSABABISHA UFOO SARO KUPIGWA RISASI NA MPENZI WAKE


Ufoo Saro (kulia) aliyepatwa na mkasa hivi punde



HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema mtangazaji wa kituo cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa risasi, huku mama yake mzazi akipoteza maisha baada ya mtu anayedakiwa kuwa mchumba wake au mumewe kuwafyatulia risasi katika ugomvi wa kimapenzi.

Taarifa zinasema kuwa mchumba wa mtangazaji huyo aliyetajwa kwa jina la Ansel aliyekuwa nchini Sudan kikazi alitua nchini jana na kufikia kwa Ufoo lakini kukatokea mzozo ambao haukupata suluhisho.

Hivyo wawili hao waliongozana hadi kwa mama wa mtangazaji huyo kutafuta suluhu, asubuhi hii na kwa bahati mbaya hali ilikuwa tete na ndipo kijana huyo alipotoa bastola aliyokuwa nayo na kumtwanga mama mtu risasi ya kichwa iliyomuua papo hapo.

Kama hiyo haikutosha inaelezwa jamaa huyo alimtwanga risasi Ufoo kifuani na nyingine mguuni na kudhani amemuua kabla ya yeye mwenyewe kujilipua mwenyewe kwa risasi ya kidevuni na kumuua.

Tayari miili ya watu hao wawili yaani mama yake Ufoo na jamaa huyo imepelekwa Muhimbili sambamba na mtangazaji huyo anayeelezwa yupo katika hali mbaya kwa ajili ya kuhifadhiwa na matibabu zaidi.

Haifahamiki chanzo cha mauaji hayo licha ya kudaiwa huenda ni ugomvi wa kimapenzi na haifahamiki jamaa huyo huko Sudan anakodaiwa kuwa alikuwa akifanya kazi UN alikuwa kama nani japo inaelezwa huenda alikuwa mwanajeshi ambapo kabla ya kwenda huko aliwahi kuwa mpiga picha wa ITV na kufanya kazi Mahakama ya Kimataifa ya Arusha kabla ya kuomba kazi UN. 
Moshono media inaendelea kufuatilia kwa kina taarifa hii na itawafahamisha. Pia inamuombea kila la heri na salama mtangazaji huyo aweze kupona katika mkasa uliopata na kumpoa pole kwa msiba uliompata kwa kumpoteza mama yake mzazi.

TUKIO KATIKA PICHA:MASKINI UFOO SARO AFANYIWA UPASUAJI WA KUONDOLEWA RISASI MWILINI APELEKWA WODI 12 YA KIBASILA.

 Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.

TAZAMA PICHA "MSIBA"NYUMBANI KWA BABA YAKE UFOO SARO‏



DSC 0107 9f37b
DSC 0108 5ec3c
DSC 0109 de82d
DSC 0110 75668
DSC 0110 ce7ee
Picha na Hudgu Ng'amilo (mjengwablog Dar)

0 comments:

Post a Comment