Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 10, 2013

MTUHUMIWA MMOJA AFARIKI DUNIA AKIWA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA TUMBONI. KYELA MBEYA


[DIWANI ATHUMANI- ACP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  WA KWANZA KUSHOTO AKIANGALIA MWILI WA MAREHEMU  KASSIM SAID KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA MBEYA
 PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZILIZOKUTWA  TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.




§  MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM  SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI.
§  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI  AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA  NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM  MUECK MICHAEL,  AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI  SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§  AWALI BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§  WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
§  KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
§  TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA  MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
§  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
                                                                              
                                                                   [DIWANI ATHUMANI- ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Post a Comment