Ni
baada ya kutuhumiwa kugushi saini zenye lengo la kushinikiza kikao cha baraza
la madiwani na kutaka kuisabishia hasala ya milioni kumi Halmashauri ya jiji la
mbeya
Meya wa jiji la Mbeya Atanasi Kapunga akiwa katika Picha mbalimbali akiongea na wananchi katika mkutano wa Hadhara
Madiwani na Viongozi wa ccm wakiwa katika mkutano wa hadhara sokomatola
Wanachama wa chama mapinduzi ccm na wananchi waliofika katika mkutano huo
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini katika mkutano
Baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kuuliza maswali katika mkutano
Habari kamili
Hatimae Madiwani
wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kufikishwa katika vyombo vya sheria
Ni baada ya
kutuhumiwa kugushi saini zenye lengo la kushinikiza kikao cha baraza la madiwani
na kutaka kuisabishia hasara ya zaidi ya milioni kumi Halmashauri ya jiji la mbeya
Hayo
yamejili katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko dogo la
sokomatola jijini hapa uliofanywa na Madiwani wote wa chama cha mapinduzi (ccm)
Akiongea
na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo Meya wa jiji la mbeya Atanasi Kapunga
amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona madiwani wa chadema wamegushi saini
na kutaka kuisababishia Halmashauri hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Aidha
Kapunga ameainisha kuwa saini hizo wamezigundua baada ya kulinganisha na zile za
madiwani wanazo saini wanapochukua posho na katika vitabu vya kula kiapo saini
hizo ni za madiwani watatu akiwemo
Diwani wa Forest Boidi Mwabulanga ambaye amelazwa katika hospitari ya Rufaa
mbeya baada ya kupata ajari Pamoja na
Mbuge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi ambaye yupo nje ya nchi.
Akiongea
Katika Mkutano huo uliandaliwa na
madiwani wote wa chama mapinduzi (ccm)
Kapunga amewataka wananchi kuwapuuza viongozi wa chadema wanaozusha maneno ya
uongo kuwa wamekula pesa kiasi cha milioni tisini na tano walipofanya safari ya
kwenda Uchina kujifunza maendeleo ya huko.
0 comments:
Post a Comment