KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI
WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILENGE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. MAGRETH D/O IJUMBA, MIAKA 55, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
ILENGE ALIUAWA AKIWA NYUMBANI KWAKE KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KISHA KUTUPWA KATIKA SHAMBA LAKE LA MIGOMBA UMBALI WA MITA 69
KUTOKA NYUMBANI KWAKE. MBINU NI KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA YA MHANGA AMBAYE
ANAISHI PEKE YAKE KUINGIA NDANI NA KUMUUA KWA KUTUMIA JIWE. AIDHA WATU HAO PIA
WALIKWENDA MTAA WA PILI NA WALIMSHAMBULIA KISA
W/O EPHRAIM, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ILENGE KWA
KUTUMIA JIWE KICHWANI NA AMELAZWA HOSPITALI YA
MISHENI IGOGWE. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII
KUACHA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA
JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
– MAUAJI.
Miili ya Marehemu ikiwa imetelekezwa katika mlima nyoka
Miili ya Marehemu baada ya kupigwa vibaya
MNAMO
TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO MLIMA NYOKA, KATA YA IGAWILO,
TARAFA YA IYUNGA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, WATU WAWILI 1. CHARLES S/O LIVINGSTONE, MIAKA 32, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA
ITEZI NA 2. TATIZO S/O MBWIGA, MIAKA
27, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA WALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE HADI
KUFA. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI T.693 CBD AINA YA SHANLEY
MALI YA KEVEN S/O MSEMWA, MIAKA 24,
MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA UYOLE.
MAREHEMU CHARLES S/O LIVINGSTONE ALIKUWA ANATOKA MAHAKAMA YA MWANZO UYOLE AKIWA MLALAMIKAJI KATIKA KESI CC 568/2013 KOSA SHAMBULIO AKIWA NI
MLALAMIKAJI NA MAREHEMU TATIZO S/O MBWAGA ALIKUWA ANAMSINDIKIZA NA WALIPOFIKA ENEO LA
UYOLE KATI WALIIBA PIKIPIKI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z.
MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
0 comments:
Post a Comment