Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu, kama ikifanikiwa kutimiza yote hayo basi kimaendeleao itazizidi klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo hadi sasa hazina hata viwanja vya maana vya mazoezi.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Mussa Mapunda anasema kuwa tayari wamenunua shamba la ekari 15 eneo la
Iwambi, Mbeya ambalo wamelitenga kwa ajili ya kujenga uwanja mkubwa wa kisasa.
Anasema, tofauti na uwanja wamepanga kujenga hosteli za kisasa watakazozitumia wachezaji wa timu kubwa, pia kwa ajili ya timu zao za vijana kuanzia umri chini ya miaka 14 hadi 20 watakaowatumia siku zijazo.
Pia watatenga eneo lingine kwenye uwanja huo kwa ajili ya kituo cha michezo. Timu hiyo kwa sasa inatumia Uwanja wa Sokoine unaomilikiwa na CCM.
Akifafanua kuhusu kuingiza nchini kontena moja la vifaa vya michezo kutoka China ambalo litakuwa na jezi, suti za michezo, kofia, skafu, bendera na soksi. Vitu hivyo vitauzwa nchini kote pamoja na nchi za Malawi na Zambia. Chanzo: Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment