Pages

Ads 468x60px

Friday, February 7, 2014

MGOGORO NDANI YA KANISA MORAVIANI TANZANIA JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAFIKIA PABAYA.

 Wajumbe wa mabaraza Ya wazee na wakristo kutoka shirika mbalimbali  watoa siku 30 Mwenyekiti arudishwe kazini.

-Wazuia Sadaka kupelekwa katika sanduku la umoja ofisi kuuza jimbo.


 WAJUMBE WA MABARAZA yA WAZEE KABLA YA KUINGIA KATIKA KIKAO WAKIBADILISHANA MAWAZO
WAKIPITIA WALAKA WANAOTEGEMEA KUPELEKWA KWA VIONGOZI WA KANISA

 WAJUMBE WAKIWA KATIKA UKUMBI WA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA JAKARANDA KABLA YA KUANZA KIKAO
KATIBU WA KIKAO CHA WAJUMBE HAO AKITOA MAELEZO YA AWALI KABLA YA KUSOMA WALAKA HUO
 MAKAMU MWENYEKITI AKIJIBU JAMBO KATIKA MKUTANO HUO

 MKUU WA MKOA ABASS KANGORO AONDOKA BAADA YA MAZUNGUZO YA SILI NA UONGOZI WA KANISA
MUANDISHI WA BLOG HII CHARLE ABARAHAM KULIA WAKITETE JAMBO NA MAKAMU MWENYEKITI ZAKARIA SICHONE
 MUANDISHI WA BLOG HII CHARLESS ARAHAM KULIA AKITAKA KUSALIMIANA NA MKUU WA MKOA ABASI KANDOLO

MWENYEKITI WA WAJUMBE HAO FRANK PHIL AKISOMA WARAKA WAO KWA MSISITIZO MBELE YA MAKAMU MWENYEKITI KANISANI HAPO

WAJUMBE BAADA YA KUMALIZA NIA YA MOYO WAO WASHIKANA MIKONO KISHA KUONDOKA


WAJUMBE WAKIWA NJE YA UKUMBI WA MKUTANO MALA BAADA YA KUIMALIZIKA MAZUNGUMZO WAKIJADILIANA JAMBO IKIWA NIPAMOJA NA KUPANGA MAKUNDI YA KUMLINDA MWENYEKITI NOSIGWE BUYA KUHAKIKISHA HAONDOLEWI KATIKA NYUMBAANAYOISHI KAMA ALIVYO PEWA BARUA YA KUHAMA IFIKAPO TAREHE 07/02/2014 
WAPO WACHUNGAJI WAKILIONA GARI HILI HUFARAHIA SANA NA WENGINE HUTOKWA NA MACHOZI UKITAKA KUJUA SILI YA USAFIRI HUU MUULIZE MCHUNGAJI WA KIMORAVIANI
                       HABARI KAMILI SOMA HAPA CHINI

MGOGORO NDANI YA KANISA MORAVIANI WAFIKIA PABAYA.


-Wajumbe wa mabaraza la wazee na wakristokuka shirika mbalimbali  watoa siku 30 Mwenyekiti arudishwe kazini.

-Wazuia Sadaka kupelekwa katika sanduku la umoja ofisi kuu.


SAKATA la mgawanyiko mkubwa ndani ya kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi, limechukua sura mpya, baada ya wajumbe wa mabaraza ya wazee na wakristo kutoka shirika mbalimbali kuandamana na kutishia kuzifunga ofisi za kanisa hilo.

Kufuatia hali hiyo wajumbe hao wametoa siku 30 kwa wasimamizi wa kanisa hilo, ambao ni Askofu Mkuu, Alinikisa Cheyo, Halmashauri Kuu na kamati tendaji ya kanisa kuitisha mkutano Mkuu wa Sinodi ili kutoa hatima ya Mwenyekiti, Nosigwe Buya, aliyesimamishwa.

Tukio hilo lilitokea jana kuanzia majira ya saa nane mchana, ambapo wajumbe hao na wakristo waliandamana hadi ofisi za jimbo la kanisa hilo eneo la Jakaranda Jijini hapa na kuweka kambi hapo wakishinikiza kikao na uongozi.

Baada ya kuona hali hiyo,Makamu Mwenyekiti, Zacharia Sichone, alilazimika kuitisha kikao hicho cha dharura kati yake na wajumbe hao wa mabaraza ya wazee, ambaowaliamua kutoa msimamo wao juu ya sakata hilo.

Kufuatia majadiliano ya zaidi ya saa tatu, wajumbe hao wa mabaraza ya wazee na wakristo hao, walitoa tamko lenye maazimio tisa kwa uongozi huo ili yaweze kutekelezwa kabla ya wao kuchukua uamuzi wa kuzifunga ofisi za jimbo hilo.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa wajumbe hao, Frank Phili, alisema walifikia hayo baada ya kubaini uongozi wa kanisa kukiuka katiba kwa kumsimamisha Mwenyekiti Buya bila ridhaa ya chombo chenye mamlaka ambacho ni(Sinodi) iliyomuweka madarakani.

“Makamu Mwenyekiti kikao cha leo kina nia ya kutafuta ufumbuzi wa maswali yafuatayo, ambayo ni chimbuko la mgogoro huu halmashauri kuu ya jimbo ya kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi(KMT-JKM) hasa Askofu (Cheyo), Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kufanya maamuzi kinyume na katiba” alisema Phili.

Alisema kama uongozi huo na bodi uliunda tume huru, ulipaswa kutoa majibu ya tume hiyo baada ya kukamilisha uchunguzi wake na kuwajulisha waumini kama barua za kumsimamisha zilivyojieleza badala ya kuendelea kukalia ripoti ya tume, licha ya kazi hiyo kumalizika kwa zaidi ya miezi mitatu.

“Kama Mwenyekiti aliyesimamishwa (Buya) alikuwa na makosa kwanini apangiwe kituo kingine cha kichungaji ?... na je Askofiu ni msemaji wa kanisa kama katiba inavyoelekeza” alihoji.

Katika taarifa hiyo, wajumbe hao wa mabaraza ya wazee na wakristo kutoka sharika mbalimbali za kanisa la moraviani, wametoa maazimio tisa yanayopaswa kutekelezwa na wasimamizi hao wa kanisa chini ya Askofu Cheyo.

Miongoni mwa maazimio hayo ni kuutaka uongozi huo wa kanisa kubatilisha mara moja maamuzi yake ya kumsimamisha kazi Mwenyekiti huyo na asihamishwe wala kughudhiwa hadi Mkutano Mkuu wa Sinodi utakapofanyika na kutoa maamuzi.

Pia wameitaka halmashauri kuu ya jimbo iwe imeitisha Mkutano Mkuu wa Sinodi  mpaka ifikapo Machi 3 mwaka huu na kwamba isipotii maazimio hayo ya wajumbe hao na wakristo watachukua hatua ya kuzifunga ofisi zote za jimbo kwa kibali baalumu kutoka serikalini.

Aidha, wamesema kutokana na hali ilivyosasa wamependekeza shirika zote kusitisha utaratibu kupeleka sadaka na matoleo yote ya sanduku la umoja katika ofisi za jimbo, ikiwemo sanduku la wilaya na maombezi hadi hapo mgogoro huo utakapomalizika.

Wakati wajumbe hao na wakristo wa kanisa hilo wakiandamana hadi ofisi hizo za jimbo na kuweka kambi ya zaidi ya saa sita kabla kukubaliwa kuwepo kwa kikao cha pamoja na Makamu Mwenyekiti, ghafla Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alitembelea kanisani hapo na kufanya mazungumzo na uongozi.

Licha ya kwamba mazungumzo yao ya siri na uongozi hayakuweza kufahamika ni wazi yatakuwa yakihusu mgogoro huo, ambapo hata hivyo baada ya kumaliza mazungumzo hayo alipanda gari na kuondoka kanisani hapo.

Mwenyekiti Buya, alisimamishwa kuendelea na shughuli za huduma tangu Julai 30 mwaka 2013 kwa tuhuma kuu mbili, ambazo  ni kutosimamia fedha za kanisa vizuri na kushindwa kutekeleza maagizo ya halmashauri kuu ya kanisa hilo.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment